Jumla
ya watu 303 wameripotiwa kuuawa katika matukio mbalimbali yakiwemo ya
kishirikina katika kipindi cha miezi sita nchini tanzania hususani katika mikoa
ya shinyanga na mara.
kwa
mujibu wa utafiti wa hali ya haki za binadamu nchini iliyotolewa leo na kituo
cha sheria na haki za binadamu jijini dar es alaam ambapo kwa kipindi hadi
june, mwaka huu, matukio hayo yameripotiwa kuongezeka.
akiwasilisha
ripoti ya kutathimini taarifa za hali na haki za binadamu
mkurugenzi wa maboresho wa kituo hicho harold sungusia amesema kwa sasa
hali si nzuri nchini tanzania ambapo vitendo vya kujichukulia sheria mkononi
vimekuwa vikiongezeka miongoni mwa jamii.
kuhusu
suala la rasimu mpya ya katiba katika kipengele cha muungano limejitokeza
katika ripoti hiyo ambapo kituo cha sheria na haki za binadamu kimewataka
wanasiasa wawaache watanzania wajadili kwa mapana katiba yao ili waweze kupata
katiba iliyo bora na si bora katiba.
wakati
huo huo, kituo hicho kimesema kipo katika hatua za mwisho za kumfikisha
mahakamani waziri mkuu mizengo pinda kufuatia kauli yake aliyoitoa
bungeni june 20 katika kikao cha bajeti ya bunge.
0 comments:
Post a Comment