Home » » Wazazi watakiwa kuwashirikisha watoto wa kike kupanga kiwango cha mahari

Wazazi watakiwa kuwashirikisha watoto wa kike kupanga kiwango cha mahari

WAZAZI na walezi wametakiwa kuacha tabia ya kupanga mahari ya watoto wao bila kumshirikisha binti husika na wakome kuchukua mahali  hiyo inayotolewa kwa ajili ya msichana kuolewa kwani wanatenda dhambi na pia ni unyanyasaji wa mtoto wa kike.

Rai hiyo imetolewa na Ustadhi kutoka taasisi ya Alqaadiria Temeke Dar esalaam sheik Ally Mkoyogore wakati alipokuwa akitoa mada mbalimba za mafundisho ya Uislamu kwa wanawake na waumini wa msikiti wa Masjid Quba Mwanalugali mjini Kibaha.

Amesema kuna baadhi ya wazazi na walezi mahari wanachukua wao na kugawana pande mbili ukeni na uumeni na kumuacha binti muhusika akiwa hajaambulia kitu zaidi ya kusubiri tu kuchukuliwa na mumewe  bila kuambulia chotechote kutoka sehemu ya mahari yake.

Mkoyogore amesema tabia hiyo imejengeka sana katika jamii na inatokana na kuendekeza mila na desturi zilizopitwa na wakati ambazo nyingi zinamkandamiza mtoto wa kike.

Sheik huyo ametumia fursa ya mafundisho hayo ya dini ya Kiislamu kuwakanya wazazi na walezi wenye tabia hiyo kuacha mara moja kwani katika kitabu kitakatibu cha Quraan mwenyezi mungu ameelekeza kuwa mahari ni haki ya binyi anayeolewa na si mtu mwingine hata kama ni baba au mama mzazi.
Awali Sheikh Mkuu wa Msikiti wa Masjid Quba na Madrasa Qiblatan Khamis Mtupa amesema wameamua kutoa mafunzo mbalimbali kwa waumini wanawake katika kipindi cha mwezi huu wa Ramadani ili kuwajengea uwezo kujua umuhimu wa kutekeleza maandiko matakatifu ya Quraan na pia kujua mamna bora ya kuishi na majirani zao.

Sheik Mtupa amesema mafunzo hayo ni ya awamu ya tatu mwaka huu na kutaja baadhi ya mada zitakazofundishwa ni pamoja na haki za wanadoa kwa mafundisho ya Uislamu ,ujasiriamali na malezi ya watoto ili wajitambue nini wanakifanya na wakisha jitambua waachane na mila na tamaduni kadhaa zilizopitwa na wakati ambazo sasa bado wanazitekeleza wakidhani wanatekeleza maelekezo ya Mungu.

Mafunzo hayo ni ya mwezi mmoja na yamefunguliwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Kiislamu ya World Islamic Call Society ya nchini Libya Sheik,Mohamed Qusuri ambaye pamoja na mabo mengine aliwasisitiza wanawake kuhubiri amani na upendo na waenzi mavazi aina ya Hijabu kwani ndiyo kinga na stara kwa mwanamke wa dini hiyo

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa