Home » » BARAZA LA KATIBA LA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA LAWASILISHA MAONI TUME

BARAZA LA KATIBA LA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA LAWASILISHA MAONI TUME



Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (katikati) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 28, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la Katiba kuhusu Katiba Mpya. Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro (kushoto kwa Jaji Warioba), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama (kulia kwa Mwenyekiti) na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela. Kushoto ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (kulia) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 28, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la Katiba kuhusu Katiba Mpya. Viongozi hao ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama (kulia kwa Mwenyekiti. Mwingine ni Katibu wa Tume Bw. Assaa Rashid.


Endelea kusoma habari hii kwa kubofya hapa chini


Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro akimkabidhi Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba (katikati) maoni ya Baraza la Katiba la Wakuu wa Mikoa na Wilaya katika ofisi za Tume leo (Jumatano, Agosti 28, 2013). Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Leonidas Gama.
Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Bw. Assaa Rashid (katikati) akiongea na Wawakilishi wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya waliofika ofisi za Tume jijini Dar es Salaam leo (Jumatano, Agosti 28, 2013) kuwasilisha maoni ya Baraza lao la katiba kuhusu Katiba Mpya. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Bw. Crispin Meela. Picha na Tume ya Katiba.

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa