Msaidizi wa Makamu wa Rais wa 
masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akimkabidhi 
Pikipiki Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Geodan Rugimbana, aliyeikabidhi 
Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya 
Makamu wa Rais, wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo katika mji huo 
mpya. Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mji Mpya wa Mabwe Pande, 
Abdallah Kunja.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, 
Geodan Rugimbana, akizungumza na wananchi wa Mji mpya wa Mabwe Pande,  
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Pikipiki kwa wananchi wa mji huo mpya,
 ambapo Mkuu wa Wilaya, alikabidhi Pikipiki hiyo kwa wananchi wa Mji 
mpya wa Mabwe pande kwa niaba ya Makamu wa Rais. 
Msaidizi wa Makamu wa Rais wa 
masuala ya Maendeleo ya Jamii, Mgeni Feruzi Kayanda, akizungumza 
machache wakati wa hafla hiyo baada ya makabidhiano.
Sehemu ya wakazi wa Mji Mpya wa Mabwe Pande waliohudhuria hafla hiyo ya makabidhiano.
Picha na OMR
 





 
 
0 comments:
Post a Comment