Kamati ya
 Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeshindwa 
kusikiliza pingamizi mbili zilizowasilishwa mbele yake dhidi ya waombaji
 uongozi wawili baada ya kukosa sifa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za
 TFF.
Kwa 
mujibu wa Ibara ya 11 (3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF, pingamizi ni 
lazima iwekwe na mwanachama wa TFF (vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, 
vyama shiriki na klabu za Ligi Kuu) au kiongozi wa kuchaguliwa wa TFF.
Pia 
pingamizi yoyote ni lazima iwe kwa maandishi ikieleza wazi sababu za 
pingamizi pamoja ushahidi wa kuunga mkono pingamizi hilo, jina kamili, 
anuani ya kudumu na kusainiwa na mweka pingamizi au Mwenyekiti/Katibu wa
 mwanachama husika.
Pingamizi
 hizo ziliwasilishwa na Shamsi Rashid Kazumari na Samwel Nyalla dhidi ya
 Wallace John Karia anayeomba kuwania nafasi ya Makamu wa Rais wa TFF na
 Vedastus Kalwizira Lufano anayeomba kuwania ujumbe wa Kamati ya 
Utendaji kupitia Kanda Namba Mbili ya mikoa ya Mara na Mwanza.
Kwa 
upande wa Kazumari ambaye alikiri hata kutowahi kuiona Katiba ya TFF 
pamoja na Kanuni za Uchaguzi, pingamizi lake halikusikilizwa kwa vile si
 mwanachama wa TFF wala kiongozi wa kuchaguliwa wa TFF. Wakati pingamizi
 la Nyalla halikusikilizwa kwa vile hakukuwa na ushahidi wowote 
uliowasilishwa, hivyo kushindwa kukidhi matakwa ya Ibara ya 11(3) ya 
kanuni husika.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
 
 
 
0 comments:
Post a Comment