Home » » HIVI NDIVYO UIVYOKUWA USIKU WA UZINDUZI WA FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU NDANI YA MLIMANI CITY

HIVI NDIVYO UIVYOKUWA USIKU WA UZINDUZI WA FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU NDANI YA MLIMANI CITY

Msanii wa muziki Lady Jay Dee aka Komando aka Anaconda akituzwa wakati akitoa burudani safi sana katika Uzinduzi wa Lulu ndani ya Ukumbi wa Mlimani city uzinduzi unaoendelea Muda huu
Elizaberth Michael (Lulu) akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa filamu ya Foolish Age iliyotengenezwa na Kampuni ya Proin Promotion chini ya Mwenyekiti wake Jonson Lukaza ambaye ameweza kujitolea kwa hali na mali mpaka kufanikisha utengenezaji wa filamu hii na uzinduzi kwa ujumla, Uzinduzi huo unafanyika usiku huu.Waigizaji wa filamu na wageni mbalimbali wakifuatilia filamu ya Lulu.Tapeli Dude akifanya mambo yake wakati wa uzinduzi huo.Mwanamuziki Barnaba Classic akiimba kwenye uzinduzi huo.Wageni waalikwa mbalimbali wakiwa katika uzinduzi huo.Elizabeth Michael (Lulu) akiwasili kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam tayari kwa uzinduzi wa filamu yake inayokwenda kwa jina la Foolish Age
Mwenyekiti wa Kampuni ya Proin Promotion akizungumza na wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa filamu ya Foolish Ege. 
Picha kwa hisani ya Lukaza Blog

**************************


UIMBAJI stadi wa Wibo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jay Dee umemjaza mahela Msanii wa Filamu aliyejizolea umaarufu kwa miaka ya hivi karibuni, Elizabeth Michael ‘Lulu’ wakati akiimba wimbo huo na Jide wakati wa uzinduzi wa Video yake mpya na yakwanza kusimama peke yake ya FOOLISH AGE.

Baada ya move hiyo kali ya dakika 120 iliyooesha ukali wa staa huyo kuoneshwa kwa dakika 20 tu na kubakisha zingine 100 kusubiri wateja kuziona majumbani kwao alipanda jukwaani kujitambulisha na kutoa shukrani kwa wamepenzi wa tasnia ya filamu nchini Tanzania kwa muitikio wao alipanda na kuimba wimbo huo wa Yahaya.

Akianzia kuimba kiitikio cha wimbo huo akiwa Back Stage, Lulu aliwashangaza watu pale alipomudu vyema wimbo huo kiasi cha mashabiki ‘Mapedeshee’ wakiongozwa na Pedeshee Rich Rich, kupanda jukwaani na kumtunza fedha kibao ambazo hakika zilimpagawisha msanii huyo na mwisho wa wimbo huo alisema mziki unalipa.

“Jamanieee kumbe mziki unalipa ile mbaya yaani  nimeimba ubeti mmoja tu hapa ona hela kibao, kuanzia sasa na mimi nitaanza kuimba mziki”, alisikika Lulu akisenma huku akishangiliwa na mashabiki wake.

Uzinduzi wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Wasanii mbalimbali walihudhuria show hiyo usiku huu pale Mlimani City
 Lulu akizungumza machache mara baada ya Move yake hiyo kuoneshwa kwa mashabiki na wapenzi wa filamu Tanzania ndani ya Ukumbi wa Mlimani City.
 Wadau walifuatilia burudani...
 Jide akikamua jukwaani...
 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
 .... Walitunzana tu kivyao vyao...

 noti alizo tuzwa Jide...

 Rich Rich akimwaga noti
 Wadau wakifuatilia uzinduzi huo wa Filamu.
 Furaha ilitawala

 Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
 Waongoza Shughuli hiyo watangazaji wa Redio na TV Double G na mwana dada kutoka Times FM walikuwepo.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA FATHER KIDEVU BLOG

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa