Bondia
Francis Cheka wa Tanzania (kulia) akimuadhibu mpinzani wake Mmarekani,
Phill Williams, wakaati wa pambano lao la raundi 12 la kuwania Ubingwa
wa Dunia uzito wa Super Middle (WBF) lililofanyika kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee usiku huu. Katika pambano hilo Bondi Mtanzania Francis Cheka ameweza kumgalagaza kwa Pointi mpinzani wake na kutwaa ubingwa huo.
*******************
Na Mwandishi Wetu
HATA
hivyo pambano hilo pamoja na yale ya utangulizi yaliingia dosari baada
ya wachezaji kama Alfonce Mchumiatumbo, aliyekuwa akizichapa na Chupac
Chipindi katika pambano lao la utangulizi la raundi sita, kugoma kupanda
ulingoni kwa kile walichokuwa wakieleza mabondia hao kuwa wanahitaji
kumaliziwa pesa zao za mkataba wa kucheza mechi hizo kabla ya kupanda
ulingoni.
Nao
mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali, pia waligoma kupanda ulingoni
wakishinikiza kumaliziwa pesa zao kwanza jambo ambalo lilifanya kuzua
taflani ukumbini hapoa huku mapambano yakichelewa kuanza.
Ilipofika
muda wa Cheka kupanda ulingoni pia alisikika mtangazaji akimuita
muandaaji wa mapambano hayo ili kufika chumba alichokuwa Bondia
mtanzania, Francis Cheka ili kumalizana naye mkwanja ili akubali kupanda
ulingoni.
Alisikika
Cheka akimuwakia muandaaji huyo kuwa, '' Nini Mmarekani hata angekuwa
Mchina, nimalizie changu kwanza ili nipande ulingoni, ambalo pia
lilichukua muda wa majadiliano hadi kuingiliwa kati na wadhamini na
wadau wa ngumi waliotangaza kujikomiti kulipa pesa hizo wanazodai
mabondia, ndipo mabondia hapo wakapanda ulingoni.
Aidha
katika pambano la raundi 10 la mabondia Mada Maugo na Thomas Mashali la
kuwania Ubingwa wa WBF wa Afrika, Thomas Mashali ameweza kumshinda kwa
pointi 2 tu mpinzani wake Mada Maugo na kutwaa Mkanda huo wa ubingwa wa
WBF wa Afrika.
Na
katika pambano la Utito wa Juu la utangulizi la Raundi sita kati ya
Bondia Alfonce Mchumiatumbo na Chupac Chipindi, Mchumiatumbo amemchapa
kwa KO mpinzani wake katika raundi ya tano, baada Chupac kunyoosha
mikono juu kuashiria na wasaidizi wake kutupa taulo ulingoni kuashiria
kushindwa kumalizia mchezo huo.
Waziri
wa Habari, Fenella Mukangara (katikati) akipozi na mabondia Phill na
Cheka, ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa pambano hilo la kimataifa.
Waziri
wa Habari, Fenella Mukangara (wa pili kushoto) akimvisha Mknda wa
Ubingwa wa Dunia wa WBF Bondia Francis Cheka baada ya kumchapa kwa
Pointi mpinzani wake Mmarekani, Phill Williams, katika pambano lao la
raundi 12 lililofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee usiku huu.
Mashabiki wa Cheka wakifurahi na kumbeba baada ya kutangazwa mshindi.
Bondia
Mmarekani Phill Williams (kulia) akichapana na Francis Cheka wa
Tanzania katika pambano lao lililomalizika usiku huu kwenye Ukumbi wa
Diamond Jubilee.
Mabondia hao wakiliana Timing.......
Cheka (kulia) na Phill wakichapana......
Cheka (kulia) na Phill,wakiendelea kuchapana
We subiri inakuja hiyooooo
Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
Sehemu ya mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kumshuhudia Cheka akimchakza Mmarekani.
Baadhi ya wageni waalikwa walioshuhudia mchezo huo.
Bondia Mada Maugo (kulia) akimwadhibu mpinzani wake, Thomas
Mashari
kwa konde zito wakati wa pambano lao la raundi 10 la kuwania ubingwa wa
Dunia wa WBF, ambapo Mashali ameibuka mshindi kwa
Pointi dhidi ya Maugo.
Chanzo: Sufiani Mafoto Blog.
0 comments:
Post a Comment