Mkurugenzi Msaidizi Uzuiaji Ujangili kutoka
Mfuko wa Kuhifadhi Wanyama Pori Bw. Paul Sarakikya akieleza kwa waandishi wa
habari kuhusu mipango ya serikali katika kupambana na ujangili na mikakati ya kulinda
hifadhi za wanyama pori nchini, Katika mkutano uliofanyika leo ukumbi wa Idara
ya Habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Habari Bi. Zamaradi Kawawa. Picha
na Frank Mvungi-MAELEZO.
======== ========= ==========
MUHTASARI
KUHUSU SHUGHULI ZA MFUKO WA KUHIFADHI WANYAMAPORI TANZANIA
1.0
UTANGULIZI
Mfuko wa
Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania (Tanzania Wildlife Protection Fund, TWPF)
ulianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 21 ya mwaka 1978 baada ya kukifanyia
marekebisho kifungu cha 69 cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori (Wildlife
Conservation Act) Na. 12 ya mwaka 1974. Marekebisho hayo yalitangazwa kwenye
Gazeti la Serikali Na. 21 la tarehe 22 Mei, 1981.
Baada ya
kufanyika mapitio ya Sheria ya Wanyamapori Na. 12 ya mwaka 1974, sheria ya
Uhifadhi wa Wanyamapori ya sasa Na. 5 ya mwaka 2009 (Sura ya 283) inabainisha
uwepo wa Mfuko kisheria katika kifungu cha 91(1). Lengo la kuwa na Mfuko ni
kuiongezea Idara ya Wanyamapori uwezo wa kifedha za kutekeleza majukumu yake ya
ulinzi wa wanyamapori. Serikali inatambua kuwa ulinzi wa wanyamapori unahitaji
fedha nyingi na fedha kutoka Hazina hazikidhi mahitaji yaliyopo.
2.0
MAJUKUMU YA MFUKO
Kwa mujibu wa
Kifungu cha 91(2) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya Mwaka 2009,
malengo ya Mfuko (TWPF) ni kuwezesha na kusaidia shughuli wanyamapori ndani na
nje ya maeneo yaliyohifadhiwa hususani katika maeneo yafuatayo:-
(i)
Uzuiaji
ujangili na usimamizi wa sheria;
(ii)
Uendeshaji
wa Kikosi cha Ulinzi wa Wanyamapori;
(iii)
Uhifadhi
wa wanyamapori;
(iv)
Kusaidia
maendeleo ya jamii zinazozunguka maeneo yaliyohifadhiwa;
(v)
Utoaji
wa elimu, mafunzo na uhamasishaji kuhusu masuala ya wanyamapori;
3.0
USIMAMIZI WA MFUKO
3.1 Bodi ya
Wadhamini ya Mfuko
Mfuko
unasimamiwa na Bodi ya Wadhamini (Board of Trustees) kwa mujibu wa kifungu cha
92 cha Sheria tajwa. Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko anateuliwa na
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Wajumbe wengine wa Bodi ambao
huingia kutokana na nyadhifa zao ni Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA), Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka za Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA),
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI),
Mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Fedha na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori ambaye ni Katibu wa Bodi. Aidha,
Wajumbe wengine wawili wa Bodi huteuliwa na Mhe. Waziri wa Maliasili na Utalii.
Bodi husimamia Mfuko katika vipindi vya miaka mitatu. Bodi iliyoko sasa ilianza
kufanya kazi Juni 2011 na inatazamiwa kumaliza kipindi chake ifikapo Juni 2014.
4.0
PROGRAMU ZILIZO CHINI YA
MFUKO
Mfuko
unagharamia uendeshaji wa program mbili zinazohusika na utoaji wa elimu ya
uhifadhi wa wanyamapori kwa jamii ndani na nje ya nchi. Programu hizo ni
“Malihai Clubs of Tanzania” na Majarida ya Kakakuona na “Tanzania Wildlife”
4.1
Malihai Clubs of Tanzania
(MCT)
“Malihai Clubs
of Tanzania” ni Programu ya Serikali chini ya Idara ya Wanyamapori
inayoshughulika na utoaji wa elimu ya Uhifadhi wa Maliasili na Mazingira katika
Taasisi za Elimu (Shule za Msingi, Kondari, Vyuo). Pia kwa mwanachama mmoja
mmoja na makundi ya jamii hasa wanavijiji wanaoishi pembezoni mwa mapori
yaliyohifadhiwa. Kwa kupitia program hii elimu ya uhifadhi kwa umma kwa vitendo
katika Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo na Vijiji hususan vile vinavyopakana na
maeneo yenye wanyamapori huenezwa.
Kwa
sasa, MCT inaendesha shughuli zake katika Kanda tatu ambazo ni:
a.
Kanda ya Kaskazini – yenye makao yake makuu katika Jiji
la Arusha
b.
Kanda ya Ziwa – yenye makao yake makuu katika Jiji la
Mwanza
c.
Kanda ya Nyanda za Juu Kusini – yenye makao yake makuu
Mbarali Mkoani Mbeya.
4.2
Majarida ya kutoa
elimu ya uhifadhi na kukuza Utalii
Mfuko
unachapisha majarida mawili: Kakakuona
ambalo ni la Kiswahili na Tanzania
Wildlife (la Kiingereza). Majarida haya ni nyenzo muhimu kwa kueneza elimu
ya uhifadhi kwa umma wa Tanzania na kutangaza utalii ndani na nje ya nchi. Pia,
ni jukwaa la wataalam mbalimbali wa uhifadhi wa Maliasili, mazingira, utalii wa
ndani na nje ya nchi. Pia, ni jukwaa la wataalam mbalimbali wa uhifadhi wa Maliasili,
mazingira, Utalii na utamaduni kubadilishana mawazo, kuelezea uzoefu na utalaam
wao. Majarida yote mawili huchapishwa mara nne kwa mwaka. Nakala 6,000 (nakala
3,000 za jarida la Kiswahili la Kakakuona na nakala 3,000 za jarida la
Kiingereza la Tanzania Wildlife) huchapishwa kila robo ya mwaka. Katika mwaka
wa fedha 2012-2013, jumla ya nakala 24,000 za majarida zilizochapishwa na
kusambazwa katika vituo vya uuzaji ambavyo viko sehemu mbalimbali nchini katika
ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii, mahotelini, kwenye baadhi ya vituo vya
Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
5.0
VYANZO VYA
MAPATO YA MFUKO
Kifungu Na.
91(3) cha Sheria ya Kuhifadhi Wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009, kimeainisha
vyanzo vya mapato ya Mfuko kama ifuatavyo:-
a.
Mapato
mbalimbali kama yatakavyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mnamo mwaka 1983, Serikali kupitia Hazina ilitoa ruzuku ya Shilingi 2,500,000/=
kama kianzio (seed money) cha Mfuko;
b.
Asilimia
25 ya mapato yatokanayo na mauzo ya wanyamapori na nyara au silaha, magari,
vyombo, ndege, mahema au kitu chochote kilichohusika katika kutenda kosa la
ujangili kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 111 cha Sheria ya Kuhifadhi
Wanyamapori Na. 5 ya Mwaka 2009. Hiki ndicho chanzo kikuu cha mapato ya Mfuko;
c.
Zawadi
na michango mbalimbali ndani na nje ya nchi itakayotolewa na wahisani, taasisi,
Serikali, au mashirika ya kimataifa; na
d.
Kiasi
chochote au mali yoyote itakayotolewa kwa Mfuko kutokana na vyanzo vingine
ambavyo vitabuniwa na Mfuko.
6.0
MIRADI/VITEGA UCHUMI VYA
KUIMARISHA MFUKO
Ili kukidhi
mahitaji ya kifedha ya uhifadhi endapo vyanzo vya sasa vya mapato vitayumba, Mfuko
umebuni miradi mbalimbali kama vyanzo vya kuongeza na/au mbadala vya mapato
(complimentary and/or alternative sources of income). Miradi hiyo ni Jengo la
Kakakuona (Kakakuona House), Pori la Akiba Pande, Bustani ya Wanyamapori
Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila (Songea) na Kambi ya kitalii katika
Pori la Akiba Selous.
7.0
CHANGAMOTO ZA MFUKO
Katika
kutekeleza majukumu yake, Mfuko unakabiliwa na changamoto mbalimbali.
Changamoto kubwa ni mbili kama ifuatavyo:
7.1
Kutokana na mabadiliko ya hali ya
kijamii na kiuchumi pamoja na kuwepo kwa teknolojia ya mawasiliano ya simu za
mkononi mahitaji ya fedha kwa ajili ya kukabiliana na wimbi la ujangili nchini
na makubwa ukilinganisha na miaka ya 80 na 90. Kutokana na hali hiyo Mfuko
hauna uwezo wa kukidhi mahitaji ya fedha kwa ajili ya kuzuia ujangili hususan
fedha za kununua vifaa vya doria (magari, radiocalls, mahema, sare), mafuta ya
magari na ndege pamoja na malipo ya posho ya kujikimu ya wahifadhi wanyamapori.
7.2
Chanzo
kikuu cha mapato cha Mfuko ni 25% ya mapato yatokanayo na biashara ya uwindaji
wa kitalii. Biashara ya uwindaji wa kitalii hutegemea wateja ambao ni matajiri
kutoka nchi za Ulaya na Marekani. Mtikisiko wowote wa kisiasa, kiamani au
kiuchumi unapotokea katika nchi ambazo watalii hao wanatoka huathiri hali ya
uwindaji nchini na hivyo mapato ya Mfuko huporomoka.
8.0
MIPANGO YA KUKABILIANA NA
CHANGAMOTO
Hatua mbalimbali
zinachukuliwa ili kukabiliana na changamoto hizo ikiwa ni pamoja na;
8.1
Kutafuta
vyanzo vingine vya mapato zaidi ya biashara ya uwindaji wa kitalii. Miradi ya
maendeleo ya Mfuko imebuniwa ili kuiendeleza na kuwa vyanzo vya mapato ya
Mfuko. Miradi hiyo ni Ujenzi wa Jengo la Kakakuona, Pori la Akiba Pande,
Bustani ya Wanyamapori ya Tabora, Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila (Songea) na
Kambi ya Utalii katika Pori la Akiba Selous Miradi hiyo iko katika hatua
mbalimbali za kuiendeleza.
0 comments:
Post a Comment