Mabondia Simba Watunduru kushoto na Ibrahimu Class 'King Class Mawe' wakitunishiana misuli wakati wa kutangaza mpambano wao.Picha na SUPER D.
Rais
wa TPBO LIMITED Yassini Abdallah 'Ostadhi' katikati akiwaamulizia
mabondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kushoto na Simba Watunduru
baada ya kusaini mkata wa kupambana August 30 katika ukumbi wa Diamond
Jubilee Dar es salaam.
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Simba Watunduru wamekiuka miko ya mchezo wa masumbwi baada ya kutaka kuchapana makonde kavu kavu mbele ya Rais wa TPBO Yassini Abdallah 'Ostadhi' wakati wa utiaji saini mkataba wa makubaliano wa kupambana mchezo wa kirafiki August 30 katika ukumbi wa Diamondi Jubilee.
Akizungumzia tukio hilo rais huyo alisema sijawai kuona vitu kama hivi vya ajabu maana vijana wamekamiana mpaka kufikia hatua ya kutaka kuchapana kavu kavu nje ya ulingo tena mbele yangu,hata hivyo mzozo huo umekubaliana kumalizika siku ya mpambano wao ambapo atajulikana nani mbabe zaidi ya mwenzake.
Nae bondia Ibrahimu Class aliyeanzisha mzozo huo ameahidi kummaliza mapema mpinzani wake ambapo anatarajia kumchakaza raundi za awali na bondia Simba nae ameahidi kumchapa class kwa K,O.
"Kiukweli kabisa huyo ni kijana mdogo sana na mmemuaisha kwangu sasa siku hiyo mimi nita mpiga K,O mbaya sana najua kuwa kwa Tanzania hii mimi ndie naongoza kuwapiga wapinzani wangu kwa K,O pindi nikutanapo nao ulingoni" alisema Simba.
Mpambano huo unatarajiwa kuwa ni mkali sana na wenye mvuto wa kipekee utakaopigwa August 30 katika ukumbi wa Diamondi Jubilee,jijini Dar es Salaam.
CHANZO: MTAA KWA MTAA BLOG
CHANZO: MTAA KWA MTAA BLOG
0 comments:
Post a Comment