Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
Jerry Silaa akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Amana Dk.Meshack Shimwela alipowasili Hospitalini hapo
kukabidhi msaada wa taa za chumba cha upasuaji kwenye Hospitalini hiyo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akizungumza
na uongozi wa hospitali ya Amana na wafanyakazi wake wakati wa hafla
fupi ya kukabidhi msaada wa taa za chumba cha upasuaji katika hospitali
hiyo inayohudumia wakazi wa Manispaa ya Ilala yenye kadirio la wakazi
1,179,992sqkm ambapo pia Hospitali ya Amana hutoa huduma kwa wakazi wa
Manispaa zingine na hata Mikoa ya Jirani.
Picha juu na chini Mstahiki Meya wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa akikabidhi rasmi
msaada wa taa hizo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Amana Dk.Meshack
Shimwela kwenye hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali
ya Amana Dk.Meshack Shimwela (kulia) kuelekea kukagua chumba cha
upasuaji katika hopspitali hiyo.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ilala Mh.Jerry Silaa kupitia wadau wake ametoa msaada wa taa
hizo zenye thamani ya shilingi Millioni sita laki saba na tisini elfu
6,790,000/= ambapo msaada huu wa taa umefika kwa wakati muafaka
utakaowawezesha madaktari
kuwahudumia wagonjwa wengi na
kupunguza msongamano mkubwa wa wagonjwa wanaohitaji huduma hiyo ambao
kwa hakika walilazimika kufanya pasuaji muda wa mchana peke yake hali
ambayo ilisababisha msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo.
Kwa upande wa huduma ya upasuaji
hospitali ya Amana inahudumia wagonjwa kati ya 20 mpaka 30 kwa siku kwa
kutumia theater mbili ambazo ni main theater na maternity theater zenye
vyumba vinne vya upasuaji (theater rooms). Kwa muda mrefu Hospitali
hiyo ilikuwa inakabiliwa na tatizo la kuharibika kwa taa ya upasuaji
(operating lamp) ambayo imepelekea kutumia vyumba vitatu vilivyopo
theater kubwa (Main theater).
(picha na habari na
--
Zainul A. Mzige)
0 comments:
Post a Comment