Katika mkutano huo na wahariri
TGNP imeainisha baadhi ya mafanikio na changamoto ambazo mtandao huo
umezipata, ikiwa mbioni kufanya tamasha la mwaka huu ambalo litafanyika
Septemba 3 hadi 6 2013, Katika viwanja vya TGNP Mabibo.
TGNP inatarajia kutumia Tamasha la
Jinsia kuwapa wanawake fursa ya kushiriki mijadala ya wazi na kupaaza
sauti zao, tamasha hili litashirikisha wanawake, wanaume, Vijana na
watoto zaidi ya 5000 kutoka mikoa yote ya Tanzania na nchi mbalimbali za
Afrika, Ulaya na Amerika.
TGNP imebainisha kuwa kupitia
Tamasha hilo, wanawake na wanaume wanaoshiriki wanapata fursa ya
kujijengea uwezo wa kutumia mbinu za kiraghibishi katika, uchambuzi wa
sera , bajeti ya kijinsia, kujadili kwa pamoja na watendaji wa serikali
kuu na za mitaa walioalikwa namna bora ya utoaji huduma ambazo
zitamfikia kila mwananchi.
Pamoja na mijadala hiyo ya wazi,
kutakuwa na mahakama ya wananchi (Popular tribunal) itakayoendeshwa na
Chama cha Majaji Wanawake (TAWJA), watunga sera, wanasheria,
wanaharakati waliobobea kwenye masuala ya Kisheria na wananchi
walioathiriwa na mfumo kandamizi na kukosa msaada wa kisheria au
kuathika na hukumu zilizotolewa. Aidha siku inayofuata kutakuwepo na
Bunge la wananchi ambalo litaongozwa na wanazuoni na wataalamu wa sheria
na wananchi wote watapata fursa ya kushiriki kikamilifu.
Mijadala mingine italenga katika
masual ya haki ya uchumi kwenye upatikanaji wa huduma za msingi za jamii
kama maji, afya, elimu, miundombinu na haki ya jamii katika umiliki wa
rasilimali ardhi. Aidha suala la Katiba mpya litapewa kipaumbele katyika
mijadala itakayopfanyika ikiwepo kuendelea kudai ushiriki ulio sawia
katika fursa na michakato iliyosalia kufikia kupata katiba mpya ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment