Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni
na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (wa pili kulia) akitoa nasaha
zake kwa Warembo wanaowania taji la Redd's Miss Tanzania 2013,wakati wa
hafla ya Chakula cha jioni ikiwa ni sehemu ya kumuaga Redd's Miss
Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto) anaetarajiwa kuondoka
hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki Mashindano ya Urembo wa
Dunia (Miss World).Hafla hiyo imefanyika usiku huu kwenye Hoteli ya
Giraffe,Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mkurugenzi wa Idara
ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Prof. Herman Mwasoko na kushoto ni Mlezi na shoto ni Mlezi wa Kamati ya
Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni
na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara (katikati) akimkabidhi Bendera ya
Taifa,Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred (pili kushoto)
anaetarajiwa kuondoka hivi karibuni kwenda nchini Indonesia kushiriki
Mashindano ya Urembo wa Dunia (Miss World 2013).Wengine pichani ni
Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Prof. Herman Mwasoko (pili kulia),Mkurugenzi Mkuu
wa Kampuni Lino International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la
Miss Tanzania,Hashim Lundenga (kulia) pamoja na Mlezi wa Kamati ya Miss
Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino
International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss
Tanzania,Hashim Lundenga akimuaga Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte
Alfred (katikati) mara baada ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa na Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo,Mh. Dkt. Fenella Mukangara
(kulia) wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kwa ajili ya kumuaga
Mrembo huyo,iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe,Jijini Dar es Salaam
usiku huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Lino
International Agency ambao ni Waandaaji wa Shindano la Miss
Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza machache ikiwa ni pamoja na kuwaasa
Warembo waliopo kambini hivi sasa kujitahidi kufanya vyema.
Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania,Mh. Emmanuel Ole Naiko akiongea machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi kuzungumza.
Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe,Dkt. Charles Bekoni akitoa salamu.
Redd's Miss Tanzania 2012/13,Brigitte Alfred akikumbatiana na Mama yake Mzazi wakati wa Kumuaga.
Redd's Miss Tanzania
2012/13,Brigitte Alfred akitoa shukrani zake wakati wa hafla hiyo ya
kumuaga iliyofanyika usiku huu kwenye Hoteli ya Giraffe,jijini Dar es
Salaam.
Sehemu ya Warembo wanaowania Taji la Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa kwenye hafla hiyo.
Picha zote na Mtaa kwa Mtaa Blog
0 comments:
Post a Comment