Home » » Rais Jakaya Kikwete amemteua Adam Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Rais Jakaya Kikwete amemteua Adam Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).


 Adam Mayingu
--
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Adam H. Mayingu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

Taarifa iliyotolewa mjini Dar es Salaam jana, Jumanne, Agosti 13, 2013, na kutiwa saini na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue inasema kuwa uteuzi unaanzia Juni 8, mwaka huu, 2013. 
Kabla ya uteuzi huo, Bwana Mayingu alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo wa PSPF.Bwana Mayingu anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, Bibi Hawa Mmanga ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria. 
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
14 Agosti, 2013

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa