Home » » SHEIKH PONDA APELEKWA SEGEREA.

SHEIKH PONDA APELEKWA SEGEREA.




Katibu wa Shura ya Maimamu, Sheikh Ponda Issa Ponda (pichani chini shati jekundu) leo  ametoka katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha  mifupa (MOI) jijini Dar es salaam alikolazwa kwa tiba ya jeraha la kinachosemekana kuwa ni risasi na kusemekana amepelekwa katika gereza la Segerea .
Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Bw. Almasi amethibitisha hilo na kusema madaktari walimruhusu Sheikh Ponda bakutoka wodini baada ya hali yake kiafya kuimarika na kuonekana hana sababu ya kuendelea kubaki hapo. 
Kuhusu habari kuwa alipigwa risasi, Bw. Almasi amesema Muhimbili walimpokea Sheikh Ponda akiwa na kidonda ambacho kilihudumiwa sehemu ingine kabla ya kupelekwa hna kwamba hawakumkuta na risasi mwilini mwake. Badala yake, alisema, walikifungua upya kidonda hicho na kukihudumia upya.

Wakati huo huo, Wakili Nassor Jumaa (pichani chini) anayesimamia Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda (54) ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mpya ya kufanya uchochezi katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amezungumzia kitendo cha kumhamisha mteja wake kutoka hositalini hadi Segerea.

Leo hii majira ya saa 7 mchana nje ya viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar  es Salaam amesema kuwa amesikitishwa na hatua  ya vyombo vya dola kumuondoa Sheikh Ponda aliyekuwa amelazwa katika wodi ya Kitengo  cha Taasisi ya Tiba  ya Mifupa  na Upasuaji wa Mishipa ya Fahamu (MOI) alikokuwa akipatiwa matibabu na kisha kumhamishia katika gereza la Segerea.

Wakili Jumaa amesema amesikitisha na kitendo hicho kwani muda mfupi baada ya wakili mwandamizi wa serikali Tumaini Kweka kumaliza kumsomea Sheikh Ponda shitaka linalomkabili, Hakimu Hellen Riwa alitoa amri ya kukaa chini ya ulinzi Sheikh Ponda aendelee na matibabu.

Jumaa akaongeza  kuwa   ameshangazwa kuona leo, wanausalama wamemtoa Sheikh Ponda wodini na kumpeleka katika gereza la Segerea na kwamba atalazimika kurudishwa tena mahakamani siku kesi yake itakapojatwa Agosti 28 mwaka huu, ambapo upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

“Kwa kweli kitendo hicho kime nisikitisha na kunishitua sana… ila tunatafakari ni hatua gani za kisheria tutazichukua huko siku za usoni,”alisema Jumaa.



 Kwa upande wao familia ya Sheikh Ponda wamesema wanalaani kitendo kilichofanywa na serikali cha kumuondoa ndugu yao hospitalini huku akiwa anaendelea kupata matibabu.

Msemaji wa familia hiyo Is-haq Rashid, alisema kutokana na hali hiyo kama familia wanalirudisha suala la Sheikh Ponda kwa uongozi wa jumuiya na Taasisi za kiislamu kwa ajili ya hatua zaidi ya kuhakikisha kiongozi mwenzao anakuwa salama.

“Uporaji huu wa mgonjwa unazidi kutupa mashaka juu ya dhamira ya serikali hasa ikiwa tunalituhumu jeshi la polisi katika kumdhuru Sheikh,hatujui kwa nini kila wakati wanafanya mambo yao kwa kuvizia kama mwanzoni tuliwaomba viongozi wenzie wawe na subira juu ya yaliyotokea sasa tunaachia hili walizungumzie wao.”alisema Is-haq.


1 comments:

Anonymous said...

sheria izingatiwe na haki za binadamu nazo zizingatiwe

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa