Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe(aliyevaa tai nyekundu), akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa
cha Usafirishani (NIT),Mhandisi Dk. Zacharia Mganilwa(kulia) leo asubuhi kabla
Waziri huyo hajakabidhi Ithibati ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo
hatarishi katika viwanja vya NIT. Kushoto
kwa Waziri wa Uchukuzi ni Mwenyektii wa Baraza la Uongozi wa chuo cha
NIT, Ms. Priscilla J. Chilipweli.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe, akitoa hotuba yake kwa wahitimu na wageni waalikwa, hawapo
pichani wakati wa sherehe ya kukabidhi Ithibati ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo
hatarishi katika viwanja vya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo asubuhi.
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe, akikabidhi Ithibati
ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa Mizigo hatarishi kwa Mhadhiri wa
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT), Bw. Juma Fimbo leo asubuhi wakati wa
sherehe maalum za kukabidhi ithibati hiyo ziliyofanyika katika viwanja vya chuo
hicho. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Dkt. Zacharia Mganilwa(wa
kwanza kushoto) na Mkuu Mwenyektii wa Baraza la Uongozi wa chuo cha NIT, Ms.
Priscilla J. Chilipweli( wa pili kushoto).
Waziri wa Uchukuzi, Dk.
Harrison Mwakyembe (wa tatu kutoka kulia waliokaa), akiwa katika picha ya
pamoja na uongozi wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji(NIT), Mwenyekiti wa Baraza
la Uongozi wa chuo cha NIT Ms. Priscilla J. Chilipweli (kulia kwa Waziri
Mwakyembe), Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi
Dkt. Zacharia Mganilwa (kushoto kwa Waziri Mwakyembe) na wahitimu wa kozi ya
kuhudumia mizigo hatarishi Bi. Dorah
John (wa kwanza kulia waliosimama) na Zuhura Adam (wa kwanza kushoto
waliosimama) wakati wa sherehe za kukabidhi rasmi Ithibati ya Kuendeshea mafunzo ya wahudumiaji wa
Mizigo hatarishi pamoja na kutunuku vyeti kwa wahitimu wa kozi hiyo. Wa kwanza
kulia waliokaa ni Mkurugenzi wa Huduma za Uchukuzi Wizara ya Uchukuzi, bw.
Peter Lupatu.
(Picha na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini-UCHUKUZI)
0 comments:
Post a Comment