Foleni
ya Waumini wakisubiri zamu yao kwenda kumjulia hali Katibu wa Jumuiya na
Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyelazwa kwenye
wodi binafsi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (Moi) akipatiwa
matibabu leo.
Katibu
Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda
amesomewa mashitaka ya uchochezi na Mwanasheria wa serikali, akiwa
wodini MOI anapoendelea kupata matibabu. Sheikh Ponda arijeruhiwa
Jumamosi iliyopita akiwa katika mhadhara wa Kiislamu huko mkoani
Morogoro. Baada ya kujeruhiwa Ponda alilazwa katika hospitali ya Taifa
Muhimbili kabla ya kuhamishiwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI)
aliposomewa mashitaka. Kesi yake itaendelea pindi atakapopata nafuu.
Lukaza Blog
Lukaza Blog
0 comments:
Post a Comment