Kwa mwendo huu, tusubiri Agosti 24 mwaka huu wakati pazia la ligi kuu litakapofunguliwa.
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wakati
harakati za kujiandaa na ligi kuu soka Tanzania bara zikiendelea kwa
klabu mbalimbali, Wekundu wa Msimbazi Simba kesho wanatarajia kucheza
mechi ya kirafiki uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam dhidi ya Kombaini
ya maafande wa Polisi.
Akizungumza na FULLSHANGWE ,
Afisa habari wa Simba, “Mr. Liverpool”, Ezekiel Kamwaga, amesema
maandalizi ya mechi hiyo yamekamilika na wachezaji wote wa klabu hiyo,
wa zamani na wapya wote wapo salama, hivyo ni nafasi kwa wanachama na
mashabiki wa klabu hiyo kwenda kuona soka la wanandinga wapya.
“Mechi
itakuwa nzuri sana, timu zote zimejiandaa vizuri, hivyo kwa wale
watakaofika uwanjani kwa watafurahia kwa maana ya matokeo au soka
maridadi”. Alisema Kamwaga.
Kamwaga
aliongeza kuwa mchezo wa kesho utawatambulisha baadhi ya wachezaji
wapya waliosajiliwa kwa ajili ya msimu ujao, lakini Amis Tambwe
hatakuwepo kwani hajawasili nchini Mpaka sasa.
“Kuhusu
Tambwe, kiukweli hatakuwepo, lakini tunatarajia kuwa naye siku ya
“Simba Day” kuonesha makali yake aliyotoka nayo katika kombe la Kagame”.
Alisema Kamwaga.
Simba
itashuka dimba la taifa kwa mara ya pili tangu kumalizika kwa ligi kuu
soka Tanzania bara mei 18 mwaka huu, ambapo mechi ya kwanza walicheza na
URA ya Uganda na kufungwa mabao 2-1, hivyo mechi hiyo ni muhimu sana
kwao kuwafurahisha wapenzi wao
0 comments:
Post a Comment