Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini
(WAMA),mama Salma Kikwete (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha ya
utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana
na rushwa ya ngono mara baada ya kukabidhiwa kitabu cha mwongozo wa
namna ya kushughulikia mashauri mbalimbali ya kisheria alichokabidhiwa
na Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania Mh. Jaji Engera Kileo leo
jijini Dar es salaam.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA)
mama Salma Kikwete akifungua warsha ya siku 1 ya utoaji Haki juu ya
kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono
iliyoandaliwa na Chama cha Majaji Wanawake Tanzania (TAWJA) leo jijini
Dar es salaam.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA)
mama Salma Kikwete (kushoto) akizungumza jambo na Bi. Salome Anyoti
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Jinsia, Usawa
na Uwezeshaji wa Wanawake leo jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Washiriki wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya
ya madaraka yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwemo waheshimiwa
Majaji wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa wakati wa
warsha hiyo ya siku 1.
Washiriki
wa warsha ya utoaji Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka
yanayoambatana na rushwa ya ngono wakiwa katika picha ya pamoja na mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) leo
jijini Dar es salaam.
Mke
wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo nchini (WAMA)
, mama Salma Kikwete (kulia) akiagana na viongozi wa Chama Cha Majaji
Wanawake Tanzania mara baada ya kufungua wa warsha ya siku 1 ya utoaji
Haki juu ya kutokomeza matumizi mabaya ya madaraka yanayoambatana na
rushwa ya ngono.
Picha na Aron Msigwa – MAELEZO
0 comments:
Post a Comment