Mkurugenzi wa Masoko na Usambazaji kutoka
Wakala wa Mbegu za Kilimo Bw. Philemon Kawamala akieleza kwa waandishi wa
habari kuhusu mchango wa wakala huo katika uzalishaji wa mbegu bora za kilimo
kwa kipindi cha misimu sita tangu kuanzishwa,wakati wa mkutano uliofanyika
ukumbi wa Idara ya Habari leo Jijini Dar es Salaam Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi
wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
3149 Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini
Mkurugenzi wa Masoko na Usambazaji kutoka Wakala wa Mbeg u za Kilimo Bw.
Philemon Kawamala(hayupo pichani). PICHA ZOTE NA FATMA SALUM-MAELEZO.
TAARIFA YA WAKALA WA MBEGU ZA KILIMO
(ASA) KWA VYOMBO VYA HABARI
Taarifa
ya wakala wa mbegu za kilimo wa Taifa (ASA) itazungumzia mambo makuu matatu
·
Mchango wa ASA katika uzalishaji wa mbegu bora kwa kipindi
cha misimu sita tangu ianzishwe
·
Aina tano za mpunga aina ya AMMKA (Aina Mpya ya Mpunga kwa
Africa) zinazopandwa kwenye maeneo ya nchi kavu (Upland rice)
·
Mfumo mpya wa
kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa wakulima kutumia mnyororo wa thamani
“ASA-APPROACH”
1.
Mchango wa ASA katika
kuzalisha mbegu bora kitaifa
Wakala wa Mbegu za Kilimo
(ASA) ulianzishwa tarehe 23 Juni, 2006 chini ya sheria ya wakala namba 30 ya
mwaka 1997. Pamoja na majukumu mengine jukukumu kubwa la wakala ni kuongeza
uzalishaji na usambazaji wa mbegu bora nchini. Msimu wa kwanza wa 2006/2007 wakala ulizalisha tani za mazao
mbali mbali 429 ambapo ilikuwa ni sawa
na asilimia 2.6 ya soko la mbegu nchini na hadi kufikia 2011/2012 uzalishaji
umeongezeka na kufikia tani 5,542 sawa na asilimia 19.79 ya soko la mbegu
nchini (angalia jedwali na.1)
Jedwali namba 1: Uzalishaji wa mbegu wa ASA
kuanzia 2006/07 hadi 2011/12.
Msimu
|
Kiasi cha uzalishaji kwa kilo
|
Kiasi
kilichozalishwa na sekta binafsi kwa kilo
|
Jumla ya kilo
zilizozalishwa kitaifa
|
Asilimia ya mchango wa ASA
kitaifa
|
2006/07
|
429,000
|
16,097,000
|
16,526,000
|
2.6
|
2007/08
|
637,000
|
16,174,000
|
16,811,000
|
3.79
|
2008/09
|
918,000
|
10,511,000
|
11,429,000
|
8.03
|
2009/10
|
1,882,000
|
14,633,000
|
16,515,000
|
11.4
|
2010/11
|
3,092,000
|
23,462,000
|
26,554,000
|
11.64
|
2011/12
|
5,542,000
|
28,000,000
|
28,000,000
|
19.79
|
2.
Aina Mpya ya Mpunga kwa
Afrika (NERICA-series)
Kamati ya mbegu ya taifa imepitisha
aina tano za mpunga wa nchi kavu aina ya AMMKA au NERICA. Kirefu cha AMMKA ni
Aina mpya ya mpunga kwa Africa au kwa kiingereza NERICA”New Rice for Africa”
AMMKA ni jina linalounganisha aina
nyingi za mpunga kwenye kundi moja. Aina hizi ni NERICA -1, NERICA-2, NERICA-4,
NERICA-5 na WAB450. Kutokana na hali ya mabadiriko ya tabia nchi na hasa ukame,
aina hizi zinavumulia sana ukame na zinapandwa kwenye maeneo yanayotegemea mvua
kama mahindi. Aina hii itachangia sana katika kuongeza uzalishaji wa mpunga
hapa nchini kwani maeneo kama haya ni mengi ikilinganishwa na mabonde ya
umwagiliaji au mabonde yanayotegemea mvua. Natumia fursa hii kuwaambia wakulima
wa Tanzania kulima aina hizi mpya za mpunga. Kwa wakulima wanaopata mvua za
muda mrefu wana nafasi ya kupanda na kuvuna mara mbili kwa mwaka kwani
zinakomaa kwa muda mfupi kwa kutumia siku 90 hadi siku 100 shambani.
3.
Mfumo mpya wa kuhamasisha matumizi ya mbegu bora kwa
wakulima kutumia mnyororo wa thamani “ASA-APPROACH”
Mnyororo wa thamani wa zao husika huanzia upatikanaji wa pembejeo, uzalishaji, kuvuna, kuongeza thamani na kuuza kwenye masoko yaliyokusudiwa. Mfumo wa zamani katika kuandaa teknolojia hadi kuifikisha kwa walengwa haukuwa ukiangalia sana mahitaji ya soko. Katika mfumo huu wa ASA wakulima na wasindikaji wanapewa aina 13 za mbegu ya mpunga na kuzitathimini kuanzia upandaji, utunzaji wa shamba, uvunaji na usindikaji na mwisho wakulima kwa kushirikiana na wafanya biashara huchagua mbegu ambayo wanajua itatoa ushindani kwenye soko na mbegu hiyo huzalishwa kwa wingi ili kukidhi mahitaji yao. Mfumo huu tulianza kuujaribu kwenye zao la mpunga na kuongeza matumizi ya mbegu kutoka tani 60 mwaka 2007 na kufikia tani 1500 mwaka 2012. Katika msimu wa 2012/13 ASA imefanyakazi na vijiji 120 katika kanda ya kati kwenye zao la alizeti ambapo tayari mwitikio kwenye matumizi ya mbegu ya alizeti unaaza kuwa mzuri ikilinganishwa na hapo awali.
0 comments:
Post a Comment