Home » » Serikali isitishe ugawaji wa vitalu vya Gesi:TPSF

Serikali isitishe ugawaji wa vitalu vya Gesi:TPSF


 Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Sekta
 Binafsi Tanzania wakiwa katika kikao cha kwanza
 tangu bodi hiyo kuteuliwa ambapo kilijadili mambo
 mbalimbali yakiwemo ya uwekezaji nchini. 
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TPSF,
 Salum Shamte akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari. 
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza. 
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta 
Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi 
akifafanua jambo wakati wa mkutano na
 waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,
 juu ya maazimio ya bodi hiyo kuhusu sera
 ya uwekezaji nchini. Kushoto ni Makamu 
Mwenyekiti wa TPSF, Salum Shamte. 

Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya Sekta

 Binafsi Tanzania (TPSF), Dk. Reginald Mengi 
akifafanua jambo wakati wa kikao cha
 kwanza tangu bodi hiyo iteuliwe. Kushoto 
ni mjumbe wa Bodi hiyo, Arnold Kileo na
 Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF, Godfrey Simbeye akizungumza.
---------------------------------------------


SERIKALI imetakiwa kusitisha mara moja mpango
 wake wa ugawaji wa leseni za vitalu vya gesi 
hadi hapo itakapopatikana sera ya gesi ili kuwapa
 fursa watanzania kumiliki vitalu hivyo.

Akizungumza na waandishi wa habari, 
Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Taasisi ya
 Uwekezaji nchini (TPSF), Dk. Reginald 
Mengi, alisema kuwa endapo ugawaji wa vitalu
 hivyo utafanyika Oktoba mwaka huu
 kama ilivyopangwa, watanzania
 hawatakuwa na uwezo wa kumiliki rasilimali hiyo.

Dk. Mengi ambaye alikuwa akizungumzia
 maazimio ya bodi hiyo iliyokutana mara
 ya kwanza jana tangu ilipoteuliwa hivi
 karibuni, alisema wakati Serikali iko
 mbioni kufanya mnada wa vitalu hivyo
 saba vya gesi, hakuna kipengere 
kinachomwezesha mtanzania kumiliki gesi hiyo.

Akizungumzia sera za uwekezaji kwa ujumla,
 Dk. Mengi alisema taasisi hiyo inaitaka 
Serikali kuingiza kwenye Katiba mpya 
inayokuja kipengere kinachowapa
 haki watanzania kuwa na ubia na
 wawekezaji wa nje badala ya kuwaachia 
wageni hao kumiliki rasilimali z
a hapa nchini kwa asilimia 100.

Alisema hali hiyo itawawezesha watanzania
 kuwa na hali ya kumiliki na kulinda 
rasilimali zao ambazo kwa sasa 
zinawanufaisha zaidi wageni kuliko watanzania wenyewe.

“Sisi tunaitaka Serikali ihakikishe kuwa
 shughuli yoyote ya uwekezaji wa kiuchimi, 
iwe na mtanzania ndani yake na watanzania hawa,
 wasishindwanishwe na wawekezaji wakubwa 
wan je,” alisema Dk. Mengi.

Naye Makamu mwenyekiti Salum Shamte,
 alisema kuwa Serikali inapaswa kuhakikisha
 sheria ya manunuzi za umma
 inawanufaisha zaidi watanzania kuliko wawekezaji.

Alisema hivi sasa kiasi kikubwa cha fedha za 
Bajeti ya kila mwaka, zinatumika katika
 kufanya manunuzi ya bidhaa na huduma 
na kazi hiyo imekuwa ikifanywa na 
wawekezaji badala ya kuwawezesha watanzania.

Akifafanua kuhusu hoja hiyo, Dk. Mengi alisema
 kuwa asilimia 80 ya Bajeti ya mwaka huu wa 
fedha, itatumika kwa ajili ya manunuzi ya
 umma hivyo ni vyema kazi hiyo ikafanywa na watanzania.

“Ukiangalia bajeti ya mwaka huu, karibu 
asilimia 80, sawa na sh trilioni 14 zitatumika
 kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa na huduma
 za umma. Fedha hizi zikiingia kwa watanzania, 
zitachangia sana kukuza uchumi wa taifa,
” alisema Dk. Mengi.

(Picha na Francis Dande Michuzi Blog)

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa