Akiwasilisha maoni ya kundi la tatu, Juma Mangora alisema Mkuu wa
Majeshi asiteuliwe na Rais, bali jukumu hilo lifanywe na Baraza la Taifa
la Ulinzi.
Mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, kuhusu Rais
kuwateua Wakuu wa Majeshi Nchini, yamezua mvutano kwa Wajumbe wa Baraza
la Katiba la Wilaya ya Liwale, Mkoani humo, wakipinga mapendekezo hayo
na wengine wakiyaridhia.
Hayo yalijitokeza juzi wakati wa mkutano wa kuijadili Rasimu ya
Mabadiliko ya Katiba Mpya na wajumbe hao kueleza kuwa Rais kuwateua
wakuu wa majeshi hawatatenda haki dhidi yake.
Baadhi walieleza Rais ni Mkuu wa Nchi hivyo jukumu hilo kutokufanywa na
yeye ni kuhatarisha usalama wa taifa na wakati wowote nchi inaweza
kupinduliwa. Akiwasilisha maoni ya kundi la tatu, Juma Mangora alisema
Mkuu wa Majeshi asiteuliwe na Rais, bali jukumu hilo lifanywe na Baraza
la Taifa la Ulinzi.
“Kama Mkuu wa Majeshi atateuliwa na Rais kutakuwa na kila hila ya kulipa
fadhila na inakuwa vigumu kumchukulia hatua kali pindi atakapokiuka
taratibu kutokana na kujuana zaidi,” alisema Mangora na kuongeza: “Ili
kuleta uwajibikaji wa Jeshi hilo, Baraza la Taifa la Ulinzi likichukua
jukumu hilo litamfanya hata Mkuu huyo wa jeshi kutokumwogopa Rais na
kutekeleza majukumu yake ipasavyo.”
Naye Mohamed Dondwa alisema Mkuu wa Jeshi la Polisi anatakiwa kupatikana
kupitia Baraza la Wakuu wa Polisi kutokana na wao kumjua yupi
anayestahili. Alisema kumpata Mkuu wa Polisi kupitia kuteuliwa na Rais
hakutakuwa na utendaji uliotukuka miongozi mwa jeshi hilo na wananchi
kuendelea kulilalamikia kutokana na kutokutenda haki kila kukicha.
Kwa upande wake, Hashim Majanjagara alisema kuwapata wakuu wa majeshi
pasipo Rais kuhusika kuwateuwa nchi inaweza kupindiliwa pasipo kujua.
“Rais ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hivyo yeye
ndiye anatakiwa kuwateuwa bila kufanya hivyo na kutumia njia nyingine
wanaweza kumsaliti kwa kushawishiwa na baadhi ya watu nan chi kuingia
katika hatari na vita,” alisema Majanjagara.
Wavutana zaidi
Wajumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya ya Liwale, mkoani Lindi,
wamevutana kuhusu uwepo wa nafasi ya mgombea huru katika Rasimu ya
Mabadiliko ya Katiba Mpya, wakieleza kuongeza wigo wa kukithiri vitendo
vya rushwa. Mjumbe wa Baraza hilo, Anord Ligai akiwasilisha maoni ya
kundi la kwanza alisema, kuwapo kwa mgombea binafsi kutasababisha kupata
kiongozi asiyekuwa na uadilifu kutokana na kutokupitia michakato ya
kumpata. Abasi Matulilo alisema, katika mambo saba ya Muungano moja wapo
ni vyama vya siasa hivyo kuwapo kwa mgombea huru kutaligawa taifa.
chanzo: Vijimambo Blog
0 comments:
Post a Comment