Aliyekuwa
Waziri wa Wizara na Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ametaka kuimarishwa kwa
utalii wa ndani kwa kutangaza vivutio vilivyopo nchini kwa maslahi ya taifa kwa
ujumla.
Maige
ametoa ushauri wake huo kupitia mtandao wa facebook huku akionyesha picha yake
akiwa Ndolezi kwenye Kimondo ambacho ni kivutio kikubwa cha utalii nchini
ambacho kinafahamika zaidi nje ya nchi kuliko ndani.
“Ni
vema kuimarisha utalii wa ndani. Hapa niko Ndolezi, Mbozi nikiangalia Kimondo!
Kwa kumbukumbu zioizoko kwenye kitabu cha wageni, eneo hili muhimu la utalii
hufikiwa na wageni 0-2 kwa siku! Tena wageni! Ni vema Wenzetu wa Maliasili
wakakitangaza zaidi” anasema Maige
Hata
hivyo kauli yake hiyo ilikosolewa na wafuasi wake katika mtandao huo wengi
wakimshangaa kwanini alishindwa kuutangaza autalii wa ndani wakati wa utawala
wake badala yake aliruhusu hata usafirishaji wa wanyama hai nje ya nchi.
Alli Kassim alihoji “wewe ulikuwa waziri kwenye wizara unayoizungumza ulifanya
nini kuhakikisha utalii wa ndani unakua au wewe ulikuwa una deal na troph
animals tu na sasa ndo unauona umuhimu wa utalii wa ndani?”
Michango
iliendelea ambapo wengi walitaka kujua alikuwa wapi kuyatumia mawazo hayo
wakati akiwa waziri.
Zuhura Hussein kaka wewe ni mmoja wa wahusika wa hii kazi tukumbushe enzi zako hili
ulifanyia kazi kwa kiasi gani ili tumshawishi kagasheki
Conrad Kihinga Wewe wakati ukiwa Waziri wa mali asili ulifanya jitihada gani
kutangaza utalii wa ndani?
Majaliwa
Mndele wanaondokaga na twiga hao angalieni hicho kimondo
watakipeleka ng’ambo siwaamini hata chembe. hadi leo isue ya twiga kitendawili
ihurumieni nchi jamani
Baraka Mwago Ulishindwaje kufanya hiyo njozi yako ukiwa naibu waziri na baadae
waziri wa Maliasili na Utalii?
Na
haya ndio yalikuwa majibu ya Maige kwa maswali hayo
Ezekiel Maige Alli Kassim, uongozi ni kupokezana kijiti. Kwa utanzania wangu nina
haki ya kushauri, kwa sasa ndiyo nafasi yangu. Hata Nyerere hakuweka lami hadi
Butiama!!! Zuhura Hussein, sidhani kama ni lazima kueleza nilifanya nini wakati
wangu ndipo nipate haki ya kushauri! Anyway, basi naondoa ushauri wangu!
Tusitangaze kimondo na vivutio vingine kwa watalii wa ndani!!! Umefurahi? Ukiwa
na msimamo wa kunibeza nadhani unajinyima advantage yangu ya uzoefu!!!!
Chanzo:
Tabianchi blog
0 comments:
Post a Comment