Home » » BODI YA BANDARI YAMUONDOA KIPANDE, MWAKYEMBE AIZUIA

BODI YA BANDARI YAMUONDOA KIPANDE, MWAKYEMBE AIZUIA


mwakyembe_f2996.jpg
Watanzania tumezoea kuburuzwa kwa upepo, na safari hii, Waziri wa Uchukuzi Harrison Mwakyembe, amekua akifanya atakavyo bila kuhojiwa kutokana na Watanzania kuzolewa na upepo wa mbwembwe zake bila kuhoji chochote.
Ni Waziri Mwakyembe ambaye aliishinikiza Bodi ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kumtimua Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Ephraem Mgawe na kumleta Madeni Kipande, lakini jana kwa mshangao ndiye ameiambia bodi ya sasa kwamba haina mamlaka ya kumtimua Mkurugenzi Mkuu wa sasa wa TPA na Kaimu Mkurugenzi wa IT, Mjumbe wa NEC bwana Magesa. Anasema sheria na kanuni haziipi mamlaka hayo bodi. Sasa Mgawe sheria ziliipa bodi mamlaka na leo sheria hiyo hiyo (akiwa Mwanasheria) haina mamlaka na hakujawahi kufanyika marekebisho yoyote.

Kwanza baada ya kikao cha Bodi cha Jumamosi kuibua hoja 22 za kumuondoa DG Kipande, kikao kikapanga kuendelea jana Jumapili katika hoteli ya Southern Sun lakini ghafla wajumbe wakaambiwa kimehamishiwa TPA Boardroom lakini Mwakyembe akakutana na Kipande na Mwenyekiti wa Bodi Southern Sun kabla ya kuja TPA na kuwafokea wajumbe wa bodi na kufunga kikao huku akiagiza kikao kijacho Bodi imfuate Dodoma watakapofanya kikao kingine. Kati ya wajumbe wanane wanne walitaka kuachia ngazi jana hiyo lakini busara ikatumika kuwambia wasubiri waone kitakachotokea. Kibaya zaidi ni Mwakyembe kuwatisha wajumbe kwamba ameongea na Rais Kikwete huko aliko na amempa nguvu ya kuwazuia Bodi wasifanye maamuzi yoyote, jambo ambalo limeelezwa kutia shaka kama kweli JK ametoa maagizo hayo akiwa nje wakati kuna Makamu na Waziri Mkuu wako nchini na halikua jambo la dharura.
Kama tunavyokumbuka Mwakyembe alikataa kufanya kazi na bodi ya zamani 7bu ilipingana naye katika taratibu nzima alizotumia za kulazimisha Bodi wausimamishe uongozi wote wa juu wa Bandari wakati huo . Siku hiyo alipolazimisha Bodi almanusra wajumbe wote wajiuzulu mbele yake ikabidi baadhi yao watumie busara kusitisha kujiuzulu huko
Ni Mwakyembe aliyeunda Kamati ya kuchunguza TPA ikilipwa fedha na TPA na kamati hiyo Mwenyekiti alilipwa 930,000 kwa siku, wajumbe 7+1 katibu kila mmoja 630,000 kwa siku na walilala na kupata huduma zote Hoteli Sourthen Sun USD 200 kwa siku (kulala tu) na walikaa kwa zaidi ya siku 60 na kuomba kuongezewa zaidi. Hadi leo ripoti ni siri maana imejaa majungu.
na Dj Sek Blog

1 comments:

Unknown said...

ngoma ikivuma sana hupasuka ndio hayo ya dokta mwakyembe maana sasa ana haribu sio kujenga tena

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa