Dar es Salaam
Wakala wa nishati vijijini REA imesaini
mkataba wa shilingi bilioni 881 na wakandarasi 16 kwajili ya utekelezaji wa
mradi wa nishati kwenye mikoa 24 ya tanzania bara .
Mradi huo unaotarajiwa kukamilika juni 2015 ni
sehemu ya mpango mkakati wa kichocheo cha maendeleo ya taifa.
Mwenyekiti wa bodi ya nishati vijijini balozi
ami mpungwe amesema mpango huo utahusisha usambazaji umeme kwenye makao
makuu ya wilaya 13 zisizo na umeme na maeneo mengine ya vijijini.
Ameongeza kuwa mpango huo umehusisha wakandarasi
kutoka ndani na nje ya nchi na pia utahusisha ujenzi wa vituo sita vya
usambazaji wa umeme vitakavyojengwa tunduru, mbinga, ngara, kigoma, kasuru na
kibondo.
Utekelezaji wa mpango huo ni juhudi za serikali
za kufanikisha mipango ya maendeleo iliyofafanuliwa kwenye dira ya maendeleo ya
taifa ya 2025 ya kufikia asilimia 30 ya nishati ya umeme kwenye maneo ya
vijijini
0 comments:
Post a Comment