Kanisa
la Kiinjili na Kilutheri KKKT limeitaka serikali kutafuta suluhu ya kudumu ya
migogoro ya ardhi inayolikabili taifa ili kuepusha migogoro inayoweza
kujitokeza kutokana na migongano ya ardhi miongoni mwa wananchi.
Benki
ya Dunia inakadiria kuwa Afrika itagharimika kiasi cha dola bilioni 4.5 kipindi
cha miaka kumi kurekebisha madhara yaliyotokana na vitendo vya ugawaji ardhi
kiholela kwa wageni.
Benki
ya Dunia inaitaja Tanzania katika ripoti zake za uchumi kuwa ni miongoni mwa
nchi kumi zinazoongoza kwa kutoa kiholela ardhi kwa wageni tena katika mchakato
usiokuwa na uwazi ambao unazidisha umasikini hasa kwenye maeneo ya vijijini.
Takwimu
kama hizo zinawapa wasiwasi wananchi na wanajamii wengine juu ya nafasi ya
wazawa katika kunufaika na rasilimali hiyo
Pamoja
na hasara hiyo ya kiuchumi, amani ya nchini nayo inakuwa mashakani kutokana na
mapambano ya kuwania ardhi ikiwa ni pamoja na mapigano ya wakulima na wafugaji.
Kamati
hiyo kupitia Taasisi ya Haki na Amani ya Sebastian Kolowa imeandaa kongamano
kubwa la kitaifa litakalofanyika wiki ijayo litakaloangazia migogoro ya ardhi
na utatuzi wake.
0 comments:
Post a Comment