Chama
cha Mapinduzi CCM kimesema mchakato wa mabadiliko ya katiba unaoendelea nchini
unahitaji uvumilivu wa kisiasa na kiitikadi ili kuepusha mivutano inayoweza kuchangia
kupata katiba isiyokuwa na maslahi kwa watanzania.
Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho Nape Nnauye ametoa kauli hiyo mbele ya
waandishi wa habari jijini Dar Es salaam huku akisisitiza kuwa ni lazima
watanzania wajue kuwa si kila jambo linalozungumzwa litaingizwa kwenye katiba.
Mivutano
baina ya vyama vya siasa, taasisi na makundi mbalimbali hapa nchini juu ya
rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 2013 ni miongoni
mwa mambo yanayomsukuma kiongozi huyu kusema yale yaliyo moyoni mwake
Tangu
ilipozinduliwa rasmi mwezi Juni mwaka huu, rasimu hiyo imekuwa gumzo hapa
nchini huku vyama vya siasa vikionyesha misimamo inayokinzana hasa katika
masuala nyeti likiwemo la muundo serikali, madaraka ya Rais na muungano.
Miongoni
mwa matukio anayoyataja ni la hivi karibuni la wabunge wa vyama vya upinzani
vya Chadema, Cuf na NCCR-Mageuzi kutoka nje ya ukumbi wa bunge kupinga muswada
wa Marekebisho ya Sheria ya Mbadiliko ya Katiba wa mwaka 2013
Wabunge
wa Bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania wanataka mjadala wa muswada huo
usitishwe kwa madai kutokuwepo na usawa kiushirikishwaji, kati ya Tanzania Bara
na Visiwani.
0 comments:
Post a Comment