Waziri
wa Ujenzi Dk. John Magufuli amepiga marufuku utoaji wa usajili wa waandisi
kwenye Bodi ya Usajili wa Waandisi nchini
ERB kabla ya kula kiapo kama sehemu ya mpango mkakati wa kupunguza
vitendo vya rushwa na kusababisha ujenzi wa majengo yaliyo chini ya viwango.
Amesema
kiapo kitawafanya wahandisi hao kujijengea uzalendo zaidi, hivyo kutoa agizo
kwa ERB kuwaapisha waandisi 13,000 waliopo nchini.
Ni
katika Mkutano wa 11 wa waandisi mbalimbali kutoka Tanzania na nchi jirani
ambapo pamoja na mambo mengine wahandisi 50 waliosajiliwa na ERB waliapishwa.
Aidha
amewataka waandisi hao kuongeza weledi kwenye kazi wanazopewa ili kuongeza
ushindani kati yao na wahandisi toka nje ya nchi.
Mwaka
1961 Tanzania ilikuwa na Wakandarasi 2, lakini idadi hiyo imeongezeka hadi
kufikia 13,000, huku bado kukiwa na changamoto ya upungufu kulingana na
mahitaji huku wakitakiwa utekelezaji wa majukumu kwa wakati.
Kamati
ya mioundombinu na Shirika la Viwango nchini TBS wanasema ipo haja kwa
wahandisi kuhakikisha viwango sahihi vya vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi ili
kuepusha madhara yatokanayo na matumizi ya vifaa vilivyo chini ya viwango.
Zaidi
ya wahandisi 1000 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wamekutana jijini Dar Es
Salaam kujadili mambo mbalimbali yahusuyo sekta hiyo ambapo miongoni mwa mada
zitakazojadiliwa ni athari za utandawazi kwa wahandisi.

0 comments:
Post a Comment