Wakili
Israel Magesa aliyekuwa mmiliki wa kampuni ya Mawakili ya Magesa
&Co. Advocates ataagwa rasmi Jumamosi 7/9/2013 katika Viwanja vya
Mnazi Mmoja, Dar Es Salaam.
Wakili
Magesa ni baba mzazi wa Phares Magesa(MNEC), Kalimba Magesa, Makongo
Magesa, Yusuh (Yohana) Magesa, Rose Magesa, Salome Magesa, Rachel
Magesa, Emmanuel (Sospeter )Magesa , Marehemu Elisha Magesa (RIP) na
baba Mkwe wa Mrs. Haika Lawere(Mkurugenzi – Mbezi Garden Hotel), Dr.
Julius Keyyu (Mkurugenzi wa Utafiti- TAWRI) na Ndg. Charanga (
Mkurugenzi – Tanzania Aviation Training College).
Marehemu ameacha mjane Rhoda
Magesa na wajukuu
8.
Wakili
Magesa enzi za uhai wake aliwahi kuwa Hakimu Mkazi Mkuu Mahakama ya
Kisutu, Katibu wa bodi na Mwanasheria Mkuu wa Benki Kuu ya Tanzania
(BOT), Msajili wa Mahakama Kuu kanda ya kusini, Mwenyekiti wa Baraza la
Nyumba Dar Es Salaam, Mwenyekiti wa Amnesty International – Tanzania
Chapter, Mwenyekiti wa Lions Club -Singida, pia ni mmoja wa wanasiasa
waanzilishi wa siasa za vyama vingi nchini.
Enzi
za uhai wake alifanya kazi ya uhakimu Mkazi mikoa ya Mbeya,
Kilimanjaro, Singida, Kagera, Mtwara na Dar Es Salaam, Wakili Magesa ni
miongoni mwa wanasheria waliomaliza shahada ya Sheria LLB katika Chuo
Kikuu Cha East Africa miaka ya sabini mwanzoni na baadae kupata shahada
ya Uzamili LLM toka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam. Pia alipata nafasi ya
kujiendeleza zaidi kimasomo katika nchi za Uingereza, Uholanzi na
Sweden.
Mipango
ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu Ukonga, Majumba Sita na
shughuli rasmi ya kuaga itafanyika Jumamosi tarehe 7/9/2013 kuanzia Saa
2-3 nyumbani kwa marehemu, saa 3-6 ibada kanisa la Mennonite
Tanzanai-Upanga, saa 6-10 jioni shughuli rasmi ya kuaga na kutoa heshima
za mwisho – Mnazi Mmoja, Dar Es Salaam na mazishi yatafanyika siku ya
jumatatu 9/9/2013 kijijini Chitare, Majita, Musoma Vijijini.
0 comments:
Post a Comment