KABLA YA DAWASCO HAWAJAFIKA WANANCHI NDICHO WALICHO KIFANYA
Mmoja wa wakazi wa mtaa huu aliye amua kujitoa na kushika kinyesi ili apate kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku Sita
Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibua
Wakazi wakiwa wanapata wakati mgumu kukatiza katika eneo hili
Zoezi la kuzibua Chemba likiwa Linaendelea katika eneo hilo ambapo wakazi wakionekana wanafanya utaratibu wa kuzizibua ..
Hali ni Tete eneo Hili ambapo sasa Chemba inazidi mwaga maji.. hapa kila mtu anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo ambalo maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka
Ilikuwa ni Baada ya Kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyo jinunulia , hatimaye walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili .
Baada ya Chemba ya Juu kuzibuka , kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.
Hapa vijana wakiulizana baadhi ya maswali ya ni jinsi gani wataanza zibua chemba ya pili
Masikini mtazame Mama huyu alivyo Ruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii... hii ni adha ya haya maji taka.
Wakazi wa eneo hili wakiwa wanakomaa kwa nguvu zote kuanza kuzibua chemba ya pili.
Zoezi sasa linaendelea na hapa walikuwa wanaendelea kuzibua chemba ya 3 ambapo sasa hapa walifika kikomo baada ya kuonekana chemba hiyo ilikuwa imejaa matakataka ya kutosha . Na ndipo walipo pata taarifa kuwa DAWASCO wanakuja.
MWANDISHI WA HABARI AMBAYE HAKUFAHAMIKA ANATOKEA CHOMBO GANI AFIKA ENEO LA TUKIO.....
Kamera yetu ilimnasa mmoja wa mwandishi ambaye hakujulikana ni wa Chombo gani cha TV akiwa anachukua picha ya maji taka hayo, lakini cha ajabu aliweza kuchukua tu eneo ambalo silo chanzo cha maji taka hayo kama inavyo onesha katika picha hapo juu.
Baada ya Kumaliza kazi zao Hao waliamua kutimka zao... Je wataenda weka habari kwa namna gani mimi na wewe hatujui.....
DAWASCO WAFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO, MIDA YA SAA NANE MCHANA
Kwa mbali sana Gari la Dawasco Linaonekana likiwa njiani kuja katika eneo la tatizo
Likikatisha Kona
Likikaribia kufika
Likiwa Limefika kabisa na kujionea Adha ya kukanyaga maji Taka ...... huo nyuma ni mtambo maalum wa kuzibua Chemba
Hapa likielekea kuanza kazi
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wamefika katika eneo la tatizo na kuanza kuzibua chemba za maji taka ili kuwasaidia wakazi hao wasipatwe magonjwa na Kero ya maji mtaani na Harufu mbaya
Wakiwa wanahakikisha kabisa kwamba tatizo limekwisha eneo hilo...
Moja ya Chemba ambayo wakazi wa Mwenge walikuwa wamehangaika nayo sana mpaka kutoa maji taka yaende ikiwa inaangaliwa na wafanyakazi wa DAWASCO
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanaendelea kutoa takataka katika chemba sugu ili kuruhusu maji yapite
Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanamalizia kufunika Chemba Mojawapo wakati Chemba Zengine 2 za eneo hilo hilo zikiwa wazi bila mifuniko.
Baada ya kumaliza kazi zao ... Hao wanaondoka zao....
Hii ni Baada ya Chemba Kuzibuliwa na wananchi wakishirikiana na DAWASCO Ambao walichelewa kufika eneo matatizo
Maji yakionekana yanaendelea kukauka baada ya Chemba hizo kuzibuliwa
Hizi ni Takataka zilizo bakia baada ya kuzibua Chemba hizo ...
Wananchi mtaa wa mwenge
waandamana na kufanya usafi kufuatiwa na kero kubwa ilyokuwa sugu na
hatari katika afya zao, kero hiyo ikiwa ni kuziba na kufumuka kwa chemba zinazo pitisha maji machafu
maarufu kama (majitaka )
Ikiwa nizaidi ya wiki mbili wakazi na watumiaji wa njia ya mwenge
katika mtaa huo uliogeuzwa jina na kupewa jina mahususi na mazingira ya mtaa
ambalo ni mtaa wa( kinyesi street) wamekumbwa na kero ya kufumuka kwa chemba za
maji taka na kuwa na harufu mbaya hivyo wananchi wamehofia afya zao nakuanza
kuzibua Chemba za maji hayo huku kila baada ya mwezi huletewa Bili na kuweza kuzilipia bila ya wasiwasi
.Lakini kibao kimegeuziwa kwa wananchi kuwa ndio wamiliki wa shirika la maji
safi na taka (DAWASCO) leo hii waamua kuondoa adha hiyo iliyo dumu kwa muda
mrefu bila ya ufumbuzi kwa kushika Kinyesi na maji machafu kutoka sehemu
mbalimbali.
Wakati jitihada za wananchi zikiendelea kikosi cha Dar es
salaam yetu Kilifika na kuweza kufanya yake
ndipo wananchi walipo lalamika kuhusu
utendaji kazi wa dawasco kuwa ni mbovu kwa kuwa wame watafuta zaidi ya
mara kadhaa bila mafanikio, Mtandao huu
uliweza kumpigia simu Muhusika wa dawasco na kuweza kufika na kushirikianana na wananchi ili kuhakikisha
kila chemba ina zibuliwa kwa uhakika .
Aidha wananchi walionekana kuwa na moyo mmoja wa ushirikiano
kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika chemba hizo nakufanikisha
kuzibua chemba zote katika mazingira magumu yanayo weza kusababisha maradhi
mbalimbali kwa jamii husika wameongeza kuwa wana iomba mamlaka ya maji
(DAWASCO) hususani kitengo cha majitaka kuweza kupita kila baada ya wiki moja
ili kuweka mazingira mazuri/safi.
0 comments:
Post a Comment