Kaimu Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya Makamu wa Rais bibi Magdalena Mtenga akimkaribisha mgeni Rasmi Injinia Angelina Madete aweze kufungua warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa haki ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete akifungua warsha ya siku mbili kwa wafanyakazi kutoka sekta mabalimbali za Serikali juu ya mafunzo kuhusu kuenea kwa Hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo leo.
Sehemu ya wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo wakiskliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete.
Wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo leo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi katika warsha hiyo Injinia Angelina Madete.
======== ======= =======
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete amesema ukame umekuwa tatizo kubwa sana katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania. Na pia umeleta athari sana katika swala zima la mazingira, ameongeza kuwa katika Africa inakadiriwa aslimia 73 ya nchi imepunguza uwezo wa kuzalisha chakula na hii imepelekea kuongezeka kwa ukame na hivyo kupelekea upungufu wa chakula Nchini.
Alitaja baadhi ya mikoa iliyoathiriwa na ukame ambayo ni Dodoma, Singida na maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga,Mara, Iringa, Manyara na Arusha. Amesema hayo leo mjini Bagamoyo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku mbili kuhusu juu ya kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa maendeleo endelevu ya ardhi.
Warsha hiyo imewashhirikisha wafanyakazi kutoka wizara mbalimbali za Serikali kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira kwa lengo kuepuka janga la ukame. Akiongea katika warsha hiyo Injinia Madete alisema kuwa ukame unaleta umaskini na pia ukame umechangia wananchi wengi kuhama maeneo yao na kwenda sehemu zingine zisizo na ukame.
Aliendelea kusema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na swala hilo la ukame amabapo mwaka 1994 ilisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupamabana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame(United Nations Convetion to Combat Dessertification UNCCD) na pia serikali inatekeleza mkataba huo kupitia Programu ya Taifa ya kupambana na kuenea kwa hali ya Jangwa na ukame(Nationala Action Programme to Combat Dessertification-NAP). Na kususdi kubwa la mkataba huu ni kuimarisha maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida aishiye kwenye sehemu za Ukame.
Warsha hiyo ya siku mbili imewashirikisha pia wadau wa mazingira kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja Wa Mataifa (UNDP).
0 comments:
Post a Comment