INAUMA SANA! Yule mtoto ambaye Amani liliripoti kuwa ndugu wanataka
auawe wiki iliyopita, Mwajuma Haji (16), amefariki dunia katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.
Mwanyuma alikuwa na ugonjwa wa kusinyaa na vipimo vya madaktari
havikuonesha ugonjwa uliokuwa ukimsumbua, ingawa viungo vyake vyote
vilikuwa vimesinyaa na kujikunja tangu alipozaliwa. Kutokana na tatizo
hilo, baadhi ya ndugu walifikia hatua ya kutaka auawe kwa walichodai
alikuwa mzigo kwa familia.
Akizungumza na mwandishi wetu kwenye mazishi ya mtoto huyo kijijini kwao
Kimange, Wilaya ya Bagamoyo, Tatu alisema mwanaye alizidiwa kwa siku
tatu mfululizo huku akiwa anapumulia mashine kabla mauti hayajamkuta.
Alisema madaktari walijitahidi kwa hali na mali kuokoa maisha yake
lakini ilishindikana kwani alikuwa akipumua kwa shida. “Mwanangu
ameteseka sana dakika za mwisho kwani kwa siku tatu mfulululizo alikuwa
akipumulia gesi tu mpaka Mungu alipomchukua,” alisema mama huyo. Katika
mazishi ya mtoto huyo, waliokuwa karibu na mama Mwajuma ni majirani zake
baada ya ndugu kuingia mitini.
Majirani wa karibu na mama Mwajuma waliliambia Amani kuwa wanasikitishwa
na tabia za ndugu zake waliosusia msiba huo na kudai ndiyo tabia yao
kwani kipindi Mwajuma alipokuwa hai walikuwa hawamjali hata walipomkuta
akinyeshewa mvua hawakumuingiza ndani hadi mama yake alipofika. “Tabia
za ndugu wa mama Mwajuma hazijaanza leo kwani walikuwa wakimtenga sana
mtoto huyo kwa kuwa hata walipomkuta ananyeshewa na mvua walikuwa
wakimuacha hadi mama yake arudi,” alisema jirani mmoja ambaye hakupenda
jina lake liandikwe gazetini.
CHANZO : VIJIMAMBO BLOG

0 comments:
Post a Comment