Dar es Salaam. Siku chache baada ya kuanzisha ukaguzi wa magari na watu wanaoingia katika maduka ya Mlimani City, ukaguzi huo sasa umesitishwa.
Hatua
hiyo ilifuatia tishio la ugaidi baada ya duka la Westgate la Nairobi
nchini Kenya kushambuliwa na kikundi cha Al-shabab na kusababisha mauaji
ya watu 68 na wengi kujeruhiwa.
Mbali
na Mlimani City lililopo Barabara ya Sam Nujoma, jijini Dar es Salaam,
maduka mengine makubwa kama vile Quality Plaza lililopo Barabara ya
Nyerere nalo lilianzisha ukaguzi kwa wateja wake.
Hata
hivyo uchunguzi wa Mwananchi hivi karibuni umebainisha kuondolewa kwa
ukaguzi uliokuwa ukifanywa kwa wateja na magari yanayoingia dukani hapo,
kwa madai kuwa unapunguza wateja.
Akizungumza
kwa sharti la kutotajwa jina gazetini, askari wa kike wa kampuni ya
Omega Nitro inayolinda duka
“Nakumbuka
Jumatano baada ya kumaliza ‘shift’ niliacha ukaguzi ukiendelea, lakini
niliporudi Ijumaa nikaambiwa umesitishwa mara moja,” alisema na
kuongeza:
“Kwa
kweli ukaguzi wenyewe ulikuwa mgumu kwani hatukuwa na vifaa vya kutosha
na wateja ni wengi,” alisema na kuongeza: “Katika ukaguzi tulikuta watu
wengi na silaha hasa bastola wakimiliki kihalali.”
Jitihada
za kuupata uongozi wa Mlimani City hazikufanikiwa kwa kile
kilichoelezwa kuwa yuko likizo. Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kinondoni, Camilius Wambura alisema hana taarifa ya kusitishwa kwa
ukaguzi, lakini akasisitiza kuwa hilo ni suala lao binafsi.

0 comments:
Post a Comment