Mwanamuziki
Profesor Jay akiwa na mfano wa hundi yenye Barcode ambazo amekabidhiwa
leo, Jay anakuwa mwanamuziki wa Pili kuchukua Barcode za Tanzania katika
sekta ya muziki wa Bongo Fleva nchini.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GS1 Tanzania Bw. Elibariki Mmari (Mwenye Koti la suti)
akizungumza wakati wa halfa fupi ya kumkabidi Barcode mwanamuziki wa
Kizazi Kipya Profesa Jay katika makao makuu ya Ofisi hiyo TIRDO Msasani
jijini Dar Es Salaam, Kulia kwa Bw. Mmari ni Fatma Kange Saleh Afisa
Mtendaji Mkuu wa GS1 Tanzania na Nd. Pius Mikongoti Afisa Muandamizi
toka GS1 Tanzania na kushoto kwa Mwenyekiti ni Bw. Joseph Haule aka
Profesa Jay.
Mwenyekiti
wa Bodi ya GS1 Tanzania Ndugu Mmari akimkabidi mfano wa hundi yenye
Barcode kwa ajili ya CD na nyimbo za mwanamuziki Pfofesa Jay huku
wajumbe wa Bodi ya GS1 Tanzania wakishuhudia.
Wanamuziki nchini wameaswa kuchangamkia fursa zilizopo kwa
kujitangaza na kutanua wigo wa mashabiki wao kwa kujiunga na huduma ya
Barcode. Hayo yamesemwa leo na mwanamuziki Profesa Jay alipokuwa
akikabidhiwa Barcode za ajili ya CD yake mpya itakayojulikana kama The
Best of Professor Jay ambayo itakuwa na mchanganyiko wa nyimbo zake
ambazo zime heat tangu kuanza kwake. “nimeamua kutoka kivingine na kwa
sasa nataka kufanya vitu kimataifa kwa kusambaza kazi zangu kwenye
mitandao ili niwafikie watu wengi zaidi” alisema Jay.
Akiongea katika makabidhiano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya GS1
Tanzania Bw. Elibariki Mmari alisema kuwa ni wakati muafaka kwa
wanamuziki wa Tanznia kuanza kuuza kwenye mitandao ya kijamii na masoko
ya kwenye mtandao kama wanavyofaidi fursa hizo wanamuziki wengine. Bwana
Mmari alisema kuwa kwa kutumia fursa hizo wanamuziki hao wanaweza kuuza
kwenye mitandao ya kijamii kwa kupitia makampuni makubwa duniani kama
CD Baby ambalo lina mikataba na maduka yote makubwa ya kwenye mtandao
kama iTune, Facebook Music na mengine makubwa.

0 comments:
Post a Comment