Sikiliza Tone Radio Tz : http://www.toneradiotz.com/listenlive.php
Mshehereshaji wa Mjadala wa wazi
ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa wenye kauli mbiu "The Future We Want"
katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa mataifa kusheherekea miaka 68 ya
kuanzishwa kwa Umoja huo akiwatambulisha Wachokonozi wa Mada Meza kuu Mh
Janeth Mbene, Naibu waziri wa Fedha (wa pili kushoto) Bi. Dorothy
Usili, Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA ( wa pili kulia), Paul Mashauri
Mwenyekiti wa East Africa Speakers Bureau ( wa kwanza kulia) na Dakta.
Lwidiko Mhamilawa, Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa
(YUNA).
.Ajira kwa vijana si bomu kama watapata mafunzo ya ujasirimali na mitaji
.Serikali yaahidi kuendelea kusaidia vijana kwa maslahi mapana ya taifa
Na Moblog Team
SERIKALI imewataka vijana kuachana na
fikra potovu za kuajiriwa pindi wanapomaliza masomo yao na badala yake
wafikiri zaidi kujiajiri ili kuweza kupambana na kuondoa kabisa tatizo
la ajira nchi. Moblog inaripoti.
Kwa muda mrefu watu wa kada
mbalimbali wasomi, viongozi wa dini na wanasiasa wameonya kwamba tatizo
la ajira kwa vijana nchini ni bomu linalosubiri kulipuka wakati wowote
kutokana na ukweli kwamba fursa za ajira zimekuwa chache nchini.
Akizungumza kwenye Mjadala wa Wazi
katika kusheherekea Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa mataifa jijini Dar
es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Janet Mbene amesema asilimia
75 ya watu hapa nchini ni vijana chini ya umri wa miaka 35 ambayo ndiyo
nguvu kazi ya taifa.
Pichani juu na chini ni Naibu
Waziri wa Fedha Bi. Janeth Mbene akitoa mada yake juu ya mstakabali wa
Vijana katika kupambana na tatizo la Ajira nchini na nafasi ya Serikali
katika kuwasaidia vijana kujikwamua kutoka katika lindi la umaskini.
‘Ni muhimu kwa vijana nchini
kutambua kwamba kwa wingi wao wanaweza kubadilisha mwelekeo wa nchi na
mustakabali wa maisha yao kwa ujumla kwa kutambua kwamba wao wana fursa
adhimu ya kufanya mabadiliko kwa maslahi mapana ya taifa,’ amesema
“Vijana wa Tanzania lazima waanze
kuchangamkia fursa za mikopo mbalimbali iliyotegwa na Serikali kupitia
Wizara ya Kazi, Ajira na Vijana kwa sababu kwa sasa Serikali si mwajiri
mkubwa kama zamani,” alisisitiza
Amesema kuwa vijana wameacha fursa
kadhaa za kujifunza na kupitia malengo na mikakati kadhaa ya Serikali
kwa sababu ya kutokupenda kujisomea na kufuatilia sera na mipango
mbalimbali ya vijana inayotolewa na Serikali.
Mbene amesema Wizara ya Fedha kupitia
benki kuu ya taifa inayo programu ya kuwawezesha vijana kiuchumi kwa
kuwapa mikopo ya ujasirimali ili waweze kujiajiri na kuondokana na
tatizo la ajira.
Amesema Serikali itaendelea
kutengeneza mazingira mazuri kwa vijana kujiajiri kwa kuwapatia mikopo,
stadi za maisha na mafunzo ya ujasirimali ili waweze kuwa wabunifu
katika biashara zao na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Mwenyekiti wa East Africa
Speakers Bureau Bw. Paul Mashauri akiwaslisha mada yake juu ya
Ujasiriamali na stadi za maisha kwa vijana ambapo pia amewasisitiza
umuhimu wa Vijana wa kutokukata tamaa kwenye biashara.
Kwa Upande wake Dakta ,Lwidiko
Mhamilawa, Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA)
amesema vijana kutokana na wingi wao wana kila sababu ya kuunganisha
nguvu zao na kupaza sauti kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Amesema kwa muda mrefu vijana
wamekuwa nyuma katika kufuatilia mipango ya Serikali kuhusu vijana na
hata sera mbalimbali zinazotungwa bungeni kwa ajili ya kundi hili vijana
wengi hawazijui.
“lazima vijana wakae chini na wajue
wanataka kwenda wapi na wako wapi na nini changamoto zao kwa sasa katika
nchi yao ili waweze kuchangia mijadala mbalimbali yenye maslahi mapana
ya nchi na wao kwa ujumla.
Dakta Mhamilawa amesema ni fursa
pekee kwa vijana kupata wasaa wa kushiriki katika mijadala mbalimbali ya
umoja wa mataifa yenye kuleta hamasa ya kujifunza kwa bidii stadi
mbalimbali za maisha.
Baadhi ya Wanafunzi wa chuo kikuu
cha Dar es Salaam wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa
zikiwasilishwa wakati wa maadhimisho hayo.
Mwakilishi Msaidizi wa UNFPA Bi.
Dorothy Usili akiwasilisha mada chokonozi ya umuhimu wa Vijana
kujitambua katika kujiletea maendeleo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwamo raia wa kigeni wakifuatilia mada hizo.
Dakta. Lwidiko Mhamilawa,
Mwenyekiti wa Asasi ya Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) akiwasilisha
mada yake ya umuhimu wa Vijana kujijengea tabia ya kujisomea na
kufuatilia sera, mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali itolewayo
kwa Vijana.
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya
Wanafunzi wa vitivo tofauti chuo kikuu cha Dar es Salaam wakiuliza
maswali wa wachokonozi wa mada.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma Ledama.
Afisa Mshiriki wa UN Cares
Beatrice Mkiramweni akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa
kutoa mafunzo ya maabukizi ya Virusi vya Ukimwi na unyanyapaa.
Afisa Mtaalamu wa Kitaifa wa
UNAIDS Bw. Emmanuel Mziray akizungumzia madhara ya unyanyapaa
yanavyoweza kuchangia maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi kwenye
sehemu za kazi na maeneo mbalimbali wakati wa mjadala wa wazi kwa Vijana
katika kusheherekea wiki ya Umoja wa Mataifa nchini uliofanyika kwenye
Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Saalaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa wakibadilishana mawazo na baadhi ya
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuhusiana na matumizi sahihi
ya Condom.
Baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa
Mataifa nje ya ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
palipofanyika mjadala wa wazi jijini Dar.
Picha na : Zainul Mzige....
0 comments:
Post a Comment