Home »
» Jaji Chande: Jamii haijui adhabu mbadala
Jaji Chande: Jamii haijui adhabu mbadala
|
|
JAJI Mkuu wa Tanzania, Othman Chande, amesema jamii haina
uelewa kuhusu adhabu mbadala inayotolewa na mahakama baada ya mtuhumiwa
kukutwa na hatia ya kutumikia adhabu ya kifungo.
Jaji Chande alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana alipokuwa
akifungua semina ya siku nane kuhusu adhabu mbadala kwa viongozi wa
nchi za Afrika.
Alisema hapa nchini adhabu mbadala ilipitishwa kama sheria na kuanza
kutumika mwaka 2002, lakini jamii katika mikoa na wilaya ambayo imeanza
kutumiwa hawaielewi kama ipo na namna inavyofanya kazi.
Alisema mikoa 17 katika wilaya 31 tayari imeanza kutumia adhabu
mbadala ambapo katika jamii iliyozizunguka mahakama hizo inalalamika
kuwa ni adhabu nyepesi.
“Jamii yetu bado ina uelewa mdogo kuhusu adhabu mbadala kwani pale
inapotolewa katika mikoa na wilaya iliyoanza kutumika wanasema ni ndogo
... hawaelewi kama inamfaa mkosaji,” alisema Jaji Chande.
Jaji Chande alisema kwa kuwa magereza hapa nchini yana wafungwa zaidi
ya 35,000 kati ya hao asilimia 30 wana makosa yanayotakiwa kutumikia
kifungo cha kuanzia miaka mitano, ambao wanapaswa kupewa adhabu
mbadala.
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma kwa Jamii, Jaji Shabani Lila, alisema
pamoja na adhabu hiyo kuanza kutumika, bado wana uhaba wa maofisa
ustawi wa jamii ambao ndio wasimamizi wakuu wa adhabu hizo.
CHANZO;TANZANIA
|
|
0 comments:
Post a Comment