Home »
» Viwanda kuinua uchumi nchini’
Viwanda kuinua uchumi nchini’
|
|
TANZANIA imeshauriwa kuimarisha miundombinu ya uzalishaji
ikiwamo uanzishwaji wa viwanda maalumu vitakavyozalisha bidhaa kutokana
na malighafi zinazopatikana nchini ili kuondokana na ongezeko la
umaskini.
Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Profesa wa Uchumi,
Charles Gore, wakati wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya Uchumi na
Jamii (ESRF), iliyokuwa ikijadili jinsi ya kupunguza ongezeko la
umaskini nchini.
Profesa Gore ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa utafiti wa UNCTAD Afrika,
alisema uanzishwaji wa viwanda utasaidia kutanua wigo wa ajira ambao
hivi sasa unaonekana kuwa changamoto kubwa nchini.
Alisema uchumi utakapoimarika serikali itaweza kutoa huduma za kijamii kama vile afya na elimu bure.
Hata hivyo, alisema bado kilimo kitabaki kuwa sekta muhimu pamoja na mapinduzi ya viwanda.
Mkurugenzi Mkuu wa ESRF, Dk. Hoseana Lunogelo, alisema semina hiyo
iliwashirikisha wadau kutoka taasisi mbalimbali za ndani na nje.
Alisema wadau hao walijadili jinsi Tanzania inavyoweza kupunguza
ongezeko la umaskini na kuleta maendeleo hususan serikali, kuwekeza
zaidi kwenye sekta ya gesi na madini.
|
|
0 comments:
Post a Comment