Home » » Kesi ya Symbion hadi Desemba 12

Kesi ya Symbion hadi Desemba 12

Dar es Salaam. Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeshindwa kusikiliza maombi yaliyofunguliwa na Kampuni ya Uwakili ya Kings Law Chambers dhidi ya Kampuni ya kufua umeme ya Symbion ikiomba ilipwe Dola 400,000 za Kimarekani kwa sababu Msajili,Amir Msumi hakuwapo.
Maombi hayo yaliyotarajiwa kuanza jana, yatasikilizwa Desemba 12,mwaka huu na Kampuni ya Kings Law Chambers ikiwakilishwa na Wakili Emmanuel Makene inaiomba mahakama hiyo iamuru kampuni hiyo ya Symbion iwalipe kiasi hicho cha fedha.
Kwa mujibu wa maombi hayo,Kampuni ya Kings Law Chambers inaomba kulipwa kiasi hicho cha fedha kama sehemu ya ada ya uwakili kwa kazi iliyoifanya ya kuiwakilisha kampuni hiyo ya kufua umeme mahakamani wakati iliposhtakiwa na Kampuni ya Mafuta ya Mogas Tanzania Ltd.
Katika kesi hiyo, Kampuni ya uwakili ya Kings iliiwakilisha Kampuni ya Symbion mahakamani na kuwekeana makubaliano kuwa kesi hiyo ikimalizika itawalipa asilimia 3 ya kiasi cha Dola 11 milioni za Kimarekani kama ada ya uwakili ambayo ni sawa na zaidi ya Sh16 bilioni.
Kampuni ya Symbion ilipaswa kuilipa Kampuni ya Kings Law Chambers kiasi cha Dola 460,000 kama sehemu ya ada ya uwakili lakini ililipa kiasi cha Dola 60 milioni zikiwa bado inadaiwa Dola 400,000 Kimarekani ambayo imesababisha kuwapo kwa maombi hayo mahakamani hapo.
Kiasi hicho cha Dola 11 milioni kilitokana na kesi iliyowahi kufunguliwa na Kampuni ya Mogas Tanzania Ltd dhidi Symbion kwa kuchukua mkopo wa mafuta i ya kiasi hicho cha fedha kwa kuendeshea mitambo ya umeme ya Dodoma, Arusha na Mwanza.
Kampuni ya Symbion baada ya kuchukua mafuta kwa mkopo yenye thamani hiyo ilishindwa kulipa,wakati ilipaswa kulipa hivyo ilipelekea kushtakiwa.

Chanzo;Mwananchi

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa