Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisaini katika Kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa mjumbe wa
Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kiongozi mwandamizi wa chama cha NCCR
Mageuzi, marehemu Dkt. Sengondo Mvungi, wakati alipofika nyumbani kwa
marehemu Kibamba Msakuzi, jijini Dar es Salaam, leo mchana kwa ajili ya
kuifariji familia ya marehemu na kutoa mkono wa pole. Mwili wa marehemu
unatarajia kuwasili nchini kesho ukitokea nchini Afrika ya Kusini.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimfariji mke wa marehemu, Dkt. Sengondo Mvungi, wakati alipofika
nyumbani kwa marehemu Kibamba Msakuzi, jijini Dar es Salaam, leo mchana
kwa ajili ya kuifariji familia ya marehemu na kutoa mkono wa pole. Mwili
wa marehemu unatarajia kuwasili nchini kesho ukitokea nchini Afrika ya
Kusini. Picha na OMR.


0 comments:
Post a Comment