Home »
» KOMBE LA DUNIA KUTUA NCHINI NOV. 29
KOMBE LA DUNIA KUTUA NCHINI NOV. 29
Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), linatarajiwa kuwasili nchini Novemba 29, mwaka huu.
Kombe
hilo linaletwa nchini na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca-Cola lengo
ni kuwa karibu zaidi na mashabiki wa soka na tukio kubwa kuliko fainali
nyingine zilizopita.
Ziara ya Kombe la FIFA la Dunia na Coca-Cola
litatoa fursa kwa mashabiki zaidi ya milioni moja kushuhudia Kombe
halisi la FIFA la Dunia katika nchi zao.
Akizungumza Dar es Salaam
jana wakati wa hafla rasmi ya kutanganza ujio wa kombe hilo Meneja Mkazi
wa Coca-Cola Tanzania Yebeltal Getachew, alisema kwamba ziara ya kombe
la dunia itatoa wasaa adimu kwa maelfu ya wapenzi wa soka jijini Dar es
Salaam kuliona kwa karibu Kombe halisi la dhahabu la FIFA la Dunia.
"Kupitia
ziara hii na promosheni nyingine kuelekea fainali za Kombe la FIFA la
Dunia 2014, Coca-Cola itasherehekea hamasa ya soka na kujaribu kuzifanya
fainali zijazo kuwa shirikishi zaidi kuliko zilizopita," alisema.
Hii
ni ziara kubwa na ndefu zaidi ya kombe la dunia. Ni ziara ya nchi 88
inayodumu kwa muda wa miezi tisa ambayo itajumuisha nchi 39 za bara la
Latin Amerika ambako ndio bara mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia
2014 ilipo. Vile vile ziara hii itajumuisha nchi 50 ambazo hazijapata
fursa ya kuwa wenyeji wa ziara ya Kombe la Dunia.
Ziara ya Kombe la
Dunia ilianzishwa kutokana na ushirikiano wa aina ya pekee uliopo kati
ya FIFA na Coca-Cola. Kampuni ya Coca-Cola ni mshirika wa FIFA wa hali
ya juu na ni moja ya washirika wa FIFA wa muda mrefu.
CHANZO;MAJIRA
0 comments:
Post a Comment