Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Selcom Wireless Tanzania, Meneja
Miradi wa Selcom, Gallus Runyeta (katikati) akitoa maelezo kuhusu
shughuli zinazofanywa na Selcom. (kushoto) ni Meneja Masoko na Muendesha
Biashara, Juma Mgori.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Selcom Wireless Tanzania, Meneja
Miradi wa Selcom, Gallus Runyeta (katikati) akitoa maelezo kuhusu
shughuli zinazofanywa na Selcom. (wa pili kushoto) ni Meneja Masoko na
Muendesha Biashara, Juma Mgori na Mhandisi wa Software, Godfrey
Kiapinga.Picha na OMR
********************************
Mheshimiwa
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib
Bilal amekutana na Uongozi wa Kampuni ya Selcomwireless Tanzania na
kufanya nao mazungumzo ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam Jumatatu
Novemba 04, 2013. Uongozi wa Selcomwireless
uliofika kukutana na Mheshimiwa Makamu ulikuwa pamoja na Meneja Miradi wa Selcom (Gallus Runyeta), Meneja Masoko na Muendesha Biashara (Juma Mgori) na Mhandisi wa Software (Godfrey Kapinga).
uliofika kukutana na Mheshimiwa Makamu ulikuwa pamoja na Meneja Miradi wa Selcom (Gallus Runyeta), Meneja Masoko na Muendesha Biashara (Juma Mgori) na Mhandisi wa Software (Godfrey Kapinga).
Wakiwa
katika mazungumzo na Mheshimiwa Makamu wa Rais, Meneja Miradi wa
Selcomwireless Tanzania Gallus Runyetta alimueleza Mheshimiwa Makamu wa
Rais kuwa, kampuni yao ambayo imejikita katika kutoa huduma za malipo ya
Kieletroniki imekuwa ikifanya miradi mbalimbali ambayo imerahisisha
malipo kwa wananchi wa Tanzania ikiwa ni pamoja na malipo ya umeme wa
Luku na sasa iko katika hatua za mwisho za kuzindua ushirikiano na
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhusu uthaminishaji wa malipo ya
magari hali ambayo itasaidia kupunguza usumbufu kwa wanaoagiza magari
nje ya nchi.
Uongozi
wa Selcomwireless pia ulimueleza Mheshimiwa Makamu wa Rais kuwa, Selcom
inazidi kujitanua katika kutoa huduma za malipo sambamba na takwimu
katika maeneo ya afya na mfano mzuri ni Zanzibar ambako huko
Selcomwireless imeshiriki katika harakati za kutokomeza Malaria,
harakati ambazo pia inashiriki kwa upande wa Tanzania Bara.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais aliwataka Selcomwireless kuendelea kuisaidia nchi hasa
katika suala zima la kukusanya mapato na akawataka kuhakikisha
wanakutana na Uongozi wa Mfuko wa Bima ya Afya ili kuwapa namna ya
kusaidia wananchi hasa wa vijijini kulipia Bima zao kwa gharama
wanazoweza kumudu.
“Mkiwasaidia
watu wa Bima ya Afya na kuwafanya walipaji kuwa wanalipa kidogo kidogo
kwa vipindi fulani inaweza kabisa kubadili hali ya huduma za afya hapa
nchini,” alisema na kuongeza: “Tunakutegemeeni sana na jitahidini
kutumia nafasi hizi ili kuhakikisha kuwa wananchi wengi wanajitokeza
kulipia Bima za afya kwa kuwarahisishia namna ya kupata huduma”.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais pia aliwataka Selcomwireless kutafuta namna ya kutatua
changamoto ya ulipaji wa kodi za nyumba sambamba na kukutana na viongozi
wa Wizara ya Ardhi, ili watu walio na Hati zao za viwanja na makazi
waweze kulipa kodi zao kwa mtandao ili kurahisisha ukusanyaji na pia
kutanua wigo wa mapato katika manispaa hapa nchini.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Ikulu, Dar es Salaam
Jumanne 05, 2013
0 comments:
Post a Comment