Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya
Hubert Kairuki Prof. Keto Mshigeni, anapenda kuwaalika wahitimu wote wa mwaka
wa masomo wa 2012/2013, wazazi, walezi wadau mbalimbali, wananchi na waandishi
wa habari, kwenye sherehe za Mahafali ya
Kumi na Moja, zitakazofanyika Jumamosi,
tarehe 2 Novemba 2013, katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,
Dar es Salaam, kuanzia Saa 3:30 Asubuhi.
Mgeni rasmi atakuwa ni Mkuu wa Chuo,
Mheshimiwa Dk. Salim Ahmed Salim, ambaye pia atatunuku vyeti, shahada, na
stashahada kwa wahitimu.
Wananchi
wote mnakaribishwa kwenye mahafali hayo.
Tangazo hili limetolewa na:
Ofisi ya Makamu Mkuu wa Chuo,
Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert
Kairuki,
S.L.P. 65300, Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255
22 2700021/4, Mob:0764378755
0 comments:
Post a Comment