Dar es Salaam.Watu watano wamefariki dunia
katika matukio tofauti, likiwemo la watu wawili waliokuwa wakiogelea
ufukweni mwa Bahari ya Hindi kuzama na kufa baada ya kuzidiwa na nguvu
ya maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo
alisema Novemba 17 mwaka huu saa 11.30 jioni eneo la Ufukwe wa Ng’onda
Kata ya Kigamboni, mwanafunzi wa Shule ya Msingi Miembeni Vingunguti,
Hajira Juma (11) akiwa na watoto kutoka kituo cha yatima Orphans wakiwa
wanaogelea, maji yalimzidi nguvu na kuzama.
Kiondo alisema watoto wa kutoka kituo hicho
walimtafuta ilipofika saa 12.15 jioni maiti yake ilionekana kandokando
mwa bahari hiyo.
Kiondo alisema Chanzo cha kifo chake inasadikiwa ni kutokuwa na ujuzi wa kuogelea na maiti imehifadhiwa Hospitali ya Vijibweni.
Katika tukio lingine, dereva wa pikipiki yenye
namba T234 CFW ambaye hakufahamika (25) akitokea Polisi Ufundi Barabara
ya Kilwa kwenda maeneo ya Bendera Tatu alipofika eneo la Mivinjeni
pikipiki yake iliwaka moto kwenye tanki la mafuta.
Kiondo alisema dereva huyo alishindwa kuimudu na kwenda kugonga kwenye gema na kufariki dunia papohapo.
Wakati huohuo, Novemba 17 mwaka huu saa 6.30
mchana eneo la Mbweni Wilaya ya Kinondoni Mkazi wa Masaki Khemi Sunder
(57) akiwa anaogelea na wenzake, maji yalimzidi guvu na kuzama.
Kamanda Camilius Wambura alisema wananchi
wanaoishi eneo hilo walifanikiwa kumuokoa akiwa hai ambapo walimkimbiza
Hospitali ya Ami iliyopo Mikocheni na kubainika kuwa ameshafariki.
Katika tukio lingine lililotokea Novemba 17 mwaka
huu saa 2.30 usiku, Mkazi wa Mbezi Makabe aliyekuwa akiendesha baiskeli
aligongwa na gari eneo la Mbezi Mwisho na kufariki dunia.
Gari iliyomgonga haikufahamika na marehemu pia hakufahamika jina lake. Maiti imeifadhiwa hospitalini.
Aidha, mkazi wa Chanika Hassan Rashid (70)
amefariki dunia baada ya kugongwa na gari lisilofahamika katika eneo la
Buyuni, Ukonga.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment