Home »
» Chiza aeleza mkakati sekta ya kilimo
Chiza aeleza mkakati sekta ya kilimo
WAZIRI wa Kilimo , Chakula na ushirika
Mhandisi Christopher Chiza ameeleza mikakati
inayofanywa na wizara hiyo kwa kuinua sekta ya kilimo hapa nchini.
Akizungumza
na Majira jana Dar es Salaam Chiza alisema Wizara ya Kilimo kwa kipindi
kirefu imepita katika changamoto ila kwa sasa
inaleta matumaini kutokana na kasi iliyopo ya kuwanufaisha wakulima wa ngazi zote.
Chiza alieleza kuwa wamekuwa wakiwaelimisha wakulima na wawekezaji kuhusu ardhi kutokana
na propaganda zinazoenezwa kwa wawekezaji wakubwa ukiwekeza katika ardhi ya Tanzania
unanyang’anywa na kutolewa kwa wakulima wadogo jambo ambalo si la kweli.
“Hizo
taarifa hazina ukweli wowote kwamba sana sana ni kuharibu sifa ya nchi
cha msingi ni wawekezaji kufika kwa wingi ili tupate mafanikio kwa
kupata ajira na hata kuongeza uchumi wa nchi,” alisema.
Waziri Chiza
alisema hivi sasa serikali ipo katika harakati mbalimbali za kuhakikisha
kuwa kilimo hapa nchini kinaendelezwa ikiwa ni pamoja na kuzungumza na
wawekezaji ili kuwaendeleza
wakulima.
“Nachotaka hivi sasa
Watanzania wafahamu kwa sasa tumezungumza na Kampuni ya Tanzania
Investment Centre (TIC) ambao wao wanachukua ardhi halafu wanawakodisha
wawekezaji ambao wakimaliza kilimo ardhi inabaki kuwa ya serikali,”
alisema Chiza.
Aliendelea kufafanua kuwa “mpaka sasa TIC ina ekari 185,000 huko Mkulanzi mkoani Morogoro
na
eka 20,000 wamezigawa kwa ajili ya kilimo cha miwa na 5,000 kwa ajili
ya kilimo cha mpunga ambapo tayari wawekezaji wameanza kujitokeza kwa
wingi.”
Chiza aliiomba TIC washirikiane na Wizara ya Kilimo ili kuweza kuinua matumaini ya wakulima Watanzania waliokuwa wameanza
kukata tamaa kutokana na kilimo kuwa na changamoto nyingi.
Hata
hivyo Chiza alisema anajua zipo changamoto katika kufikia Mpango wa
Matokeo Makubwa Sasa (Big Result Now) ila anafarijika kutokana na
wakulima sasa kuanza kuelewa umuhimu wa mpango huo
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment