Dar es Salaam. Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika leo
anakutana na wananchi wenye makazi pembezoni mwa barabara ya Morogoro
waliothirika na nyongeza ya hifadhi kinyume cha sheria ya ardhi na amri
ya Mahakama Kuu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya
mbunge huyo, mkutano huo utakaohusisha pia kamati ya waathirika wa
hifadhi ya barabara pamoja na wananchi wengine kutoka majimbo ya Ubungo,
Kisarawe na Kibaha utafanyika eneo la Luguruni Makondeko.
Mkutano huo umekuja kutokana na kamati ya
waathirika wa hifadhi ya barabara kumwandikia barua Mnyika na kumweleza
uamuzi wa Mahakama Kuu ambayo iliamua kuwa eneo hilo wanalimiki kihalali
na walipewa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Wananchi hao wamekuwa na malalamiko ya haki zao za
msingi za makazi na za kibinadamu kuvunjwa kwa maagizo kutoka kwa
Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli ambayo hutekelezwa na Tanroads.
Kwa nyakati mbalimbali katika ya mwaka 2011, 2012
na 2013 yamejitokeza malumbano ndani na nje ya Bunge baina ya Mbunge
Mnyika akiwakilisha wananchi na Magufuli akisisitiza msimamo wa serikali
kuhusu utata wa upana wa barabara ya Morogoro na haki za wananchi.
Katika mkutano huo, mbunge atasikiliza malalamiko
ya wananchi juu ya hatua ya Wizara ya Ujenzi na Tanroads bila kujali
hukumu ya mahakama .
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment