Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makala, akisaini Kitabu cha Wageni katika Ofisi za
DAWASA. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El Maamry
na Kulia ni Mkurugenzi wa DAWASA, Archad Mutalemwa. Mkurugenzi
wa DAWASA, Archad Mutalemwa akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Maji,
Amos Makala na katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA, Said El
Maamry. Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala, akizungumza katika mkutano alipotembelea DAWASA. Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya
DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya DAWASCO. Afisa
Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala akimwonyesha ripoti ya
DAWASCO, Naibu Waziri wa Maji, Amos Makala na kushoto ni Mwenyekiti wa
Bodi ya DAWASCO.
………………………………………………………………………..
Naibu
Waziri wa Maji, Amos Makala jana alitembelea DAWASA na DAWASCO
kuzungumza na uongozi wa taasisi hizo nchini zenye dhamana ya kusimamia
huduma za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na miji midogo ya Kibaha na
Bagamoyo.
Mhe.
Makala ametembelea taasisi hizo na kuzungumza na menejimenti na bodi za
taasisi hizo ili kufahamu maendeleo na utendaji wa taasisi hizo katika
kuleta matumaini ya huduma bora za maji katika mkoa wa Dar es Salaam na
mji midogo wa Kibaha na Bagamoyo.
“Tuna
chanagamoto ya upatikanaji wa maji, lakini kama Serikali ni jukumu letu
kuhakikisha tunalipatia ufumbuzi ”, alisema Naibu Waziri wa Maji, Amos
Makala.
“Hatuna
budi kuweka mikakati sahihi na kutekeleza kwa kasi miradi inayoendelea
ili wananchi wapate maji na waliopewa dhamana ya usimamiaji watekeleze
kwa wakati”, alisema Naibu Waziri.
Pia,
Mhe. Makala amedhamiria kutatua tatizo sugu la wizi wa maji na
kuhakikisha hatua za kisheria zinachukuliwa kwa wahusika na akasisitiza
wahusika lazima wachukuliwe hatua kali.
Aliongeza
suala la upotevu wa maji liwe ni ajenda ya kudumu ili kuhakikisha
linakwisha na kuziasa DAWASA na DAWASCO zisiwe chanzo cha matatizo, bali
watafute ufumbuzi wa tatizo la maji.
Mkurugenzi
wa DAWASA, Archad Mutalemwa alisema DAWASA imeweka mikakati ya upanuzi
wa mitambo na mifumo ya maji, ujenzi wa bwawa la Kidunda na kuthibiti
maji yanayopotea kuhakikisha inaboresha huduma zake.
Aidha,
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Jackson Midala alisema mikakati
waliyojiwekea ni kupunguza madeni wanayodai wateja wake, kufunga mita
kwa wateja wote na kuongeza uzalishaji ili kuongeza ufanisi wa mamlaka
hiyo.
Hii
ni mara ya kwanza tangu Mhe. Makala ateuliwe kuwa Naibu Waziri wa Maji
kutembelea taasisi hizo zinazotoa huduma ya maji jijini Dar miji midogo
wa Kibaha na Bagamoyos.
Ziara hiyo itaendelea kwa Naibu Waziri wa Maji kutembelea miradi ya maji ya Ruvu Chini na Juu na maeneo ya Segerea na Ubungo.
0 comments:
Post a Comment