Moto ulizuka jana katika ghorofa ya nne katika Jengo la GMC
Heights lililopo Barabara ya Nyerere umeteketeza vitu vyote
vilivyokuwamo katika chumba ambacho kinatumika kama stoo ya kuhifadhi
santuri (CD) za muziki na stika zake.
Moto huo ambao chanzo chake hakijafahamika ulizuka
saa 7:45 mchana katika jengo hilo ambalo lina ghorofa saba na kuzua
mtafaruku mkubwa kwa majirani na watu wengine wanaotumia jengo hilo.
Kaimu Kamanda Polisi Temeke, Ibrahim Kihongo
ambaye alikuwapo eneo la tukio alisema ni mapema mno kuweza kuzungumzia
moto huo ila ni kweli umetokea.
Kaimu Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Ukoaji
Wilaya ya Temeke, Uli Mbuluko alisema moto huo wamefanikiwa kuudhibiti
baada ya kulazimika kufanya kazi ya ziada kuweza kuufikia baada ya
kukuta mizigo ya santuri na karatasi za lebo zake.
“Tulifika mapema muda mfupi baada ya moto kuanza
kuwaka lakini hata hivyo haikuwa rahisi kufika eneo ambako moto ulikuwa
unawake kutokana na kukuta mizigo mingi katika ngazi,” alisema.
Kaimu kamanda huyo alibainisha kuwa chanzo cha moto huo hakijajulikana na haukujeruhi.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment