Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), ambaye pia
ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, (CHADEMA), Zitto Kabwe, akiwa na Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaam Jumatano Januari 29,
2014, akikagua vitabu vya ziada. Kamati ya bunge ya PAC, ilifanya ziara
ya kushtukiza shuleni hapo ili kubaini kama vitabu vilivyonunuliwa
kutokana na chenji ya rada vimekwishagawiwa kwenye shule mbalimbali kama
ilivyoahidi serikali. Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, kamati yake
ilikuta vitabu hivyo vikitumiwa na wanafunzi.
Zitto akizungumza na wanafunzi
Wanafunzi wakipiga makofi, wakati mwenyekiti huyo akizungumza nao
Wanafunzi wakisikiliza maelezo ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za serikali (PAC), ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini
(CHADEMA), Zitto Kabwe, kwenye shule ya msingi Bunge katikati ya jiji la
Dar es Salaam Jumatano Januari 29, 2014
0 comments:
Post a Comment