Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza
Chiza alisema jijini Dar es Salaam kuwa ni lazima TRA wawe wakali na wahakikishe njia zote zinazotumika kuingiza bidhaa zisizo halali zinadhibitiwa kutokana na kuwapo wafanyabiashara wasio waaminifu. Kuhusu viwanda vya sukari, Chiza alivionya kwamba visitumie nafasi hiyo kufungia sukari viwandani ili iadimike halafu baadaye wapandishe bei.
Alisema kiwanda kitakachofanya hivyo kwam makusudi ya kuwaumiza wananchi kitachukuliwa hatua kali.
Chiza alisema: “Tumefanya hivyo kuvisaidia viwanda ili viwalipe wafanyakazi mishahara mizuri, lakini tumejiridhisha kuwepo kwa sukari ya kutosha na ndiyo maana ukienda katika maduka utakuta bei ni Shilingi 1,800 na 2,000, kwa hiyo tunaamini kama TRA watadhibiti mianya yote, ni lazima tufikie malengo,” alisema. Wakulima wadogo wa miwa wameupongeza uamuzi huo wa serikali.
Oswadi Paul, mkulima wa miwa Kilombero alisema: “Kwa sasa wizara inafanya maamuzi yenye busara, ndiyo maana leo (juzi) sisi tunafurahia uamuzi huo.”
CHANZO:
NIPASHE
0 comments:
Post a Comment