Home » » Majina 2,722 yawasilishwa Ikulu Bunge la Katiba

Majina 2,722 yawasilishwa Ikulu Bunge la Katiba

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue
Ikulu imesema kuwa hadi sasa makundi yaliyowasilisha mapendekezo katika bunge la Katibu ni 575 na majina 2,722.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, alisema jana kuwa taasisi zisizo za kiserikali zina nafasi 20 katika bunge hilo.

Taasisi za kidini ambazo zina nafasi 20 katika Bunge la Katiba, zilizopeleka majina ni 77 na zimewasilisha majina 277.

Kundi lingine ni la vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu vyenye viti 42 na vilivyowasilisha mapendekezo ni 21 pamoja na majina 126.
Alisema taasisi za elimu zina nafasi 20, lakini zilizowasilisha ni tisa sambamba na majina 82.

Balozi Sefue alifafanua kuwa makundi ya watu wenye ulemavu wenye viti 20 na kwamba makundi yaliyopeleka mapendekeko ni 24 sambamba na majina 70. Balozi Sefue alisema vyama vya wafanyakazi vina nafasi 19, lakini vilivyowasilisha mapendekezo ni 20 sambamba na majina 69. Kundi lingine ni vyama vinavyowakilisha wafugaji vina nafasi 10, makundi yaliyopeleka mapendekezo ni manane sambamba na majina 43.

Alisema vyama vinavyowakilisha wavuvi vina nafasi 10 na vilivyopeleka mapendekezo ni saba sambamba na majina 45. Alifafanua kuwa vyama vya wakulima vina nafasi 20, lakini vilivyopeleka mapendekezo ni 22, sambamba na majina 115.

Menye yenye malengo yanayofanana yana nafasi 20, lakini yaliyowasilisha mapendekezo ni 142 na majina 710. 
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported byBlogs za Mikoa
Copyright © 2012. Dar es salaam Yetu - All Rights Reserved
Designed by Blogs za Mikoa
Proudly powered by Blogs za Mikoa