WATANZANIA wameshauriwa kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya hapa nchini kutokana na kuwa na ubora wa hali ya juu.
Mwito
huo ulitolewa jana na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha G&B Soap
Industries Ltd, Godliving Makundi, wakati wa utambulisho wa dawa mpya ya
meno Family dent kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa Watanzania wengi wamekuwa na tabia ya kuthamini na kupenda bidhaa
zinazozalishwa kutoka nje ya nchi na kuacha bidhaa zinazozalishwa katika
viwanda vya ndani ambapo kwa sasa ni bora zaidi ikilinganishwa na hapo
awali.
" Nikasumba tu ndugu zangu, ukweli ni kwamba viwanda vya hapa
nchini huzalisha bidhaa bora zaidi kuliko zinazoagizwa kutoka nje hata
kama ukienda TBS (Shirika la viwango) utapata jibu la haya
ninayowaambia,"alisema Makundi.
Pia alisema Watanzania wengi
wanapoteza ajira nyingi kwani viwanda vingi haviwezi kuzalisha kutokana
na kukosa soko ambalo limetawaliwa na bidhaa nyingi kutoka nje, hivyo ni
rai kwa serikali kuviunga mkono viwanda vya nchini kwa kuweka kodi
ndogo ili vizalishe bidhaa nyingi kwa bei nafuu na bidhaa kutoka nje
ziwekewe na kodi kubwa ili serikali isipoteze fedha nyingi za kigeni kwa
ajili ya uagizwaji wa bidhaa kutoka nje.
Kuhusu dawa mpya ya meno ya
Family dent, Bw.Makundi alisema kwamba kutokana na tatizo la meno kuwa
kubwa hapa nchini ujio wa dawa hiyo ni ukombozi kwani ina nguvu sita
ambazo ni kupambana na utando mdomoni, kung'arisha meno, kuzuia kuoza
kwa meno, kuimarisha fizi pamoja na kuondoa harufu mbaya ya kinywa.
Aliongeza
kuwa Family dent ipo katika mifumo miwili wa kawaida na herbal itakuwa
ni suluhisho na itakuwa historia kwaWatanzania kusumbuka na matatizo ya
meno.
Alisema kuwa watumiaji wada wa hiyo wanatakiwa kujiamini kwa
sababu hata madaktari wa meno nchini, Shirika la Viwango nchini, TBS,
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) wamelithibitisha hilo na kuwapa hati
ya uthibitisho.
Vilevile alisema kuwa licha ya ushindani
wakibiashara uliopo kampuni yake imejipanga kukabilia nao kwa kuzalisha
bidhaa bora kwa bei nafuu pia kutosheleza soko la ndani na muda mfupi
ujao Family dent itaanza kuuzwa nje ya nchi kwa lengo la kuipatia
serikali fedha za kigeni na kuongeza ajira kwa Watanzania .
Amezitaja
nchi hizo kuwa ni Burundi, Kenya, Msumbiji Malawi, Uganda, Rwanda,
Sudani ya Kusini, Congo na kwa siku za baadaye nchi za Ulaya pia.
0 comments:
Post a Comment